Hebu tuzungumzie kidogo ishu ya Vanessa Mdee..

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Karibuni,

Nimekutana na taarifa 'njema' ambazo zinamhusisha msanii wetu pendwa, Vanessa Mdee ambaye alishawahi kuitwa Central na Makonda, kwamba amepata dili nono la kusaini na Lebo ya Kimataifa ya Muziki (Universal Music Group), akiwa ni msanii wa kwanza kutoka Afrika kupata dili hilo..



Kwa lugha nyepesi, Vanessa amesainiwa na Lebo namba moja duniani ambayo inasimamia wanamuziki nyota na mahiri maarufu wakiwemo Jay Z, Elton John, Rihanna, Lady Gaga, Mariah Carey, Lil Wayne, Kanye West, Adele nna wengine wengi..

Yaani, hakuna msanii ambaye amewahi kusaini na lebo hiyo halafu asifanikiwe kukua kimuziki duniani. Hakuna.

Kwa ufupi, Vanessa anaenda kuwa kundi la wasanii namba 1 mashuhuri na tajiri duniani (A-List Artists)

Ifahamu hii lebo kwa undani Universal Music Group, the world's leading music company | Home Page - UMG

Mnasemaje; tumpongeze au tumzodoe?!
 
Hongera yake kama usemavyo ni kweli
 
Msanii wa kwanza v money?

Ina maana mondi alitudanganya?

maana mondi alitupa taarifa za kusaini mkataba kitambo sana, iweje leo useme v.money ndio msanii wa kwanza?
 
nampongeza. apige kazi ya waswahili mazito
 
Diamond na yy kasainiwa ama alikuwa anatudanganya?
Nimeshangaa kusikia v.money ndio wa kwanza
Msanii wa kwanza v money?
Ina maana mondi alitudanganya? Maana mondi alitupa taarifa za kusaini mkataba kitambo sana, iweje leo useme v.money ndio msanii wa kwanza?
---------
Neno KUMZODOA halina nafasi kwenye hii taarifa yako.

Unaweza kusema tena hilo neno halina nafasi? Sikuwa mjinga kuandika hivyo.
 
Diamond na yy kasainiwa ama alikuwa anatudanganya?
Diamond alisha sign universal vanessa afrika sio wa kwanza na wala mondi sio wa kwanza.

kuna wengine walishasign kama burna...p-square...na gazza music hawa ni wanamibia[production]

Mkumbuke wana tawi lao South Africa, America, central europe, nchi nyingi zaidi ya 70.

Hongera kwa vanessa.
 
Kwanini tumzodoe?
Wanakujaga hivi hivi... Oh dili la maana.. Mkwanja mrefuuu... Kumbe matumaini hewa!

Na Diamond ashawahi kusema amesaini nao na mapichapicha aliweka, inakuwaje huyu aseme ndio msanii wa kwanza kutoka Afrika kusaini?

Nataka wazodoaji wakusanye taarifa nyingine zaidi... Kama hakuna, tutampongeza. Wasiwasi wangu tusijetoa pongezi feki, hazisaidii..
 
Msanii wa kwanza v money?

Ina maana mondi alitudanganya?

maana mondi alitupa taarifa za kusaini mkataba kitambo sana, iweje leo useme v.money ndio msanii wa kwanza?
Nimemsikia Vannesa amefafanua kwamba kuna universal Africa ni branch ambayo nadhani ndio kina Mondi na wengineo kutoka Africa wamesign
Ila yeye amesaini na Universal main(Europe) ambayo yeye anakuwa wa kwanza kutoka pande hizi hii ni kwa mujibu wa maelezo yake na uelewa wangu
 
Napenda sana iwe hivi kweli.. Lakini nikikumbuka yale ya Sony na Rose Muhando au Kiba naishiwa nguvu..
 
Aache porojo kama magufuli na yeye. Cha muhimu ni lebo,
 
at end of the day, wewe binafsi akisha zodolewa unafaidika nini?
 
Diamond alisha sign universal vanessa afrika sio wa kwanza na wala mondi sio wa kwanza.

kuna wengine walishasign kama burna...p-square...na gazza music hawa ni wanamibia[production]

Mkumbuke wana tawi lao South Africa.

Hongera kwa vanessa.
Kwahyo huyo demu katulisha matango pori?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…