Pre GE2025 Heche: Hatutatoa nafasi kwa kuangalia uchawa

Pre GE2025 Heche: Hatutatoa nafasi kwa kuangalia uchawa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Makamu Mwenyekiti wa wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, John Heche amesema chama hicho kitashirikiana na kila mwanachama na yeyote mwenye nia ya kufanya nacho kazi bila kuangalia aliwaunga mkono yeye au Mwenyekiti wa sasa Tundu Lissu katika kipindi uchaguzi.

Akizungumza leo Januari 29, 2025 kwenye mapokezi ya Mwenyekiti wa chama hicho Tundu Lissu, Makao Mkuu ya chama hicho Mikocheni Dar Es Salaam, Heche amesema "Hakuna mtu atapata upendeleo kwa sababu alimuunga Lissu mkono na Heche, tutachagua watu kutokana na uwezo, uwezo wako utakuweka kwenye nafasi tulihubiri mabadiliko na tutasimamia mabadiliko hakuna mtu ataonewa kwa sababu hakutuunga mkono kuweni na amani kabisa."


Soma, Pia: Tundu Lissu, John Heche na viongozi wengine wapokelewa Ofisi za CHADEMA Makao Makuu. Wasisitizia No Reform, No Election
 
Nani alitoa nafasi kwa kuangalia uchawa?

Mnajenga nyumba moja hizi kauli haziwezi kuponya majeraha.
 
Bila machawa nchi itanuna sana 🙆🏻‍♀️Mbona uongozi utakuwa mgumu sana.
 
Ni mwendo wa meritocracy tu!

Kweli Chadema saivi ndo inatengeneza njia.
 
Back
Top Bottom