Sasa kiongozi Mkubwa hivyo wa chama anapigwa kama ngoma hawa wengine watakua na hali gani?Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, Heche John, amesema kuwa yule aliyehusika kumpiga Katibu Mwenenzi wa Baraza la Wanawake wa Chadema (BAWACHA) Taifa, Sigrada Mligo, achukuliwe hatua za kisheria.
Pia, Soma: Ghasia Ndani ya CHADEMA: Mwenezi wa BAWACHA Taifa ashambuliwa na Walinzi wa Heche
Heche John ameyasema hayo katika mahojiano na Elolama FM akieleza juu ya tukio la kupigwa kwa kiongozi huyo Machi 25, 2025, mjini Njombe.
Sahihi kabisaHeche alikuwepo kwenye tukio na si Heche tu hata viongozi wengine kwahiyo hao ndiyo mashuda wazuri wakumtea swala hilo likienda mahakama na siyo hao POLISI waliompeka nyumbani kwake.Hili swala ni la kisiasa na Nadhani huyu Sigranda alikuwa anajua ni nini hatima yake ndani ya Chama kwahiyo akawa anatafuta tension ili ionekane kuwa hata maamuzi yakitoka ionekane Anaonewa kwakuwa yeye ni timu Pinzani na mwenyekiti wa sasa. Kikubwa Lisu afanye kikao cha dharula ndani ya chama, cha kuhakikisha anaponya majeraha ya uchaguzi mkuu na kunapatikana muafaka kwa team zote mbili kwa sababu team mbowe wanaona kama wanabaguliwa na kuchukiwa ndani ya Chama ni wengi wao wanaonekana kama walichukua fedha kama wenje. kikubwa kikao cha upatanisho na maridhiano kinatakiwa kifanyike nchi nzima hasa Jimbo la kaskazini pamoja na wenyeviti woto wa mikoa na majembo. Ingawa kikao hicho kitakuwa siyo rasmi na hakipo kwenye katiba.Kinapaswa kiratibiwe vizuri na ili kiweze kuleta manufaa badala yakuongeza majeraha. Tundu Lisu aelewe mchuano wa uchaguzi ulikuwa mkali sana na uliacha maumivu makali sana kwa upande ulioshindwa kwa sababu haukutegemea kushindwa.
Kiongozi Mwandamizi anapigwa kama Ngoma,wafuasi wao watakua na hali gani?๐๐Hili suala linakiathiri kuliko unavyofikiria. CDM ilipaswa kulizima mapema ili kuzuia CCM kulitumia kisiasa. Na tayari wanalitumia kupakazia chama kizima wakati nyie mnajifanya hamuoni.
Hamna mvutano maana kila mtu anajua Team Lissu ilishinda uchaguzi. Hao unaowaita Team Mbowe hawana mamlaka yeyote ndani ya Chadema. Ni wajibu wa Team Lissu kuwaonyesha kuwa pamoja na wao kushinda uchaguzi, wale walioshindwa bado wana nafasi na heshima katika chama. Kuwananga ni siasa mbovu.
Tangu lini kuwa Team Mbowe imekuwa dhambi? Mlitaka wote wawe Team Lissu? Kama kigezo cha kumuamini mtu ni kumkubali Lissu basi tatizo ni kubwa. Wanaokiharibu chama chenu sio CCM bali ni wale wanaotaka kutumia nafasi zao au ukaribu wao na viongozi kulipa visasi. Sagrida sio mnafik. Anachotaka ni heshima wanayostahili kama viongozi. Aidha, anakataa kubagaza mchango mkubwa wa Mbowe kwa chama chake. Kufanya hivyo sio kukataa kuutambua uongozi wa sasa.
Kama mna imani hiyo hapatakuwa na kuponya vidonda. Hivi unadhani Mbowe angetaka kuendelea kama Mwenyekiti angeshindwa? Amesaidia kufanikisha uchaguzi uliokuwa huru na haki na amempisha Mwenyekiti mpya aongoze chama. Tofauti na unavyosema, ni Team Lissu ndio inaelekea haikutegemea kushinda maana wanajua ni vigumu wa viongozi wa vyama vya siasa nyumbani kukubali kushindwa. Walijua Mbowe atatumia hata mbinu chafu kubaki madarakani. Alipoendesha uchaguzi ambao kila mtu ameusifia na kukubali kushindwa iliwastua. Kinachosikitisha ni kuwa badala ya kuhakikisha chama kinabakia kimoja, baadhi yao wanaendekeza siasa za visasi na kuchafuana.
Approach ya Mbowe na Lissu ni tofauti. Hata hivyo hamna kampeni ya chama ambayo Mbowe hakujihusisha kikamilifu.
Sio dhambi kujitayarisha kugombea ili kama uongozi ukibadili mawazo au mabadiliko ya maana yakifanyika wawe katika nafasi nzuri ya kushinda nafasi za kutosha. Ni kuwaonea kuwashutumu kuwa watakuwa tayari kutumika ili mradi tu wapate ushindi. Mtazamo huo ndio unaharibia chama chenu. CCM haishindwi kuweka mtu ambae hata sio mwanachama wa CDM kugombea. Aidha, wanaweza kuhakikisha wagombea kutoka vyama vingine vitakavyoshiriki kwenye uchaguzi vinashinda. Kama ilivyofanywa kwa Chaumma. Vyama kama CUF, NCCR Mageuzi hata ACT-WAZALENDO havitajivunga nafasi hiyo ikitokea.
Amandla...
Inahitaji hekima na busaraUsisahau kuwa Lissu alimpigia debe sana na kwa wazi mshindani wake Sharifa? Alipaswa kuhakikisha kuwa anapewa heshima anayostahili na hahujumiwi kama ambavyo yeye anavyotaka wale ambao walikuwa upande wa pili wamheshimu. Bawacha ni nguzo muhimu ya CDM na wakiisononesha itakula kwao. Kuna hasara gani kwa Makamu Mwenyekiti kwenda hospitali kumjulia hali Katibu Mwenezi wa Bawacha? Jambo hilo lingepunguza sana tension unayoisema kuliko watu kushinda mtandaoni kumchafua Sigrada.
Amandla...
Bado zinafanya kazi haswaMaigizo ya pesa za Mama Abdul hayo
๐ฎ๐ฎ๐ฎHao watakuwa mashuhuda wa mlinzi na sio wa Sigrida kama polisi watamfungulia Noel mashtaka. Heche na hao viongozi wengine inaelekea hawako neutral kwenye suala maana wanaonekana tayari wana matatizo na Sigrida. Huwezi kuwaita mashuhuda wazuri kwa sababu hiyo. Polisi waliokuwa kwenye tukio la kupigwa Sigrida wataaminiwa zaidi na Mahakama maana kesi ni kupigwa kwa Sigrida sio yaliyotokea kwenye kikao.
Kama tayari mmeisha mhukumu na mna mpango wa kumshughulikia kabla hata ya kumsikiliza kwa sababu tu ni Team Mbowe basi yuko sahihi kuona kuwa anaonewa na uongozi uliopo. Na kama unachosema ni kweli wenye tatizo ni Team Lissu kwa sababu wanaendekeza visasi badala ya kujaribu kuwavuta wale ambao walikuwa upande wa pili.
Kikao cha kuponya majeraha cha nini kama tayari mnawatuhumu kuwa walihongwa? Hilo la Wenje mpaka sasa hivi hamjatoa ushahidi wowote kuwa alihongwa ingawa mnazo taarifa zote.
Unajichanganya. Hicho kikao hakitasaidia kitu kama hamtakubali ukweli kuwa waliompinga Lissu walikuwa na haki ya kufanya hivyo na hivyo wapewe heshima zao kama wanachama wengine. Kuwabagua na kuwafanyia fujo hakutatibu hayo majeraha. Wanapolalamika kuwa wanaonewa wasikilizwe na zichukuliwe hatua za dhati za kuzuia upuuzi huo. CDM bado inawahitaji sana.
Amandla...