Pre GE2025 Heche: Tumekaa kimya kuepusha mpasuko zaidi ndani ya chama, wakati muafaka ukifika nitatoa mwelekeo wangu

Pre GE2025 Heche: Tumekaa kimya kuepusha mpasuko zaidi ndani ya chama, wakati muafaka ukifika nitatoa mwelekeo wangu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu,

images - 2024-12-21T100226.296.jpeg

Heche ameandika haya kwenye ukurasa wake wa X

Tuna jukumu la kihistoria la kuhakikisha tunaipatia Nchi yetu chama mbadala, na serikali mbadala itakayowatumikia watu na kuwaondoa katika umasikini wa miaka 63 ya Uhuru.

Serikali na chama kitachopinga rushwa bila aibu, chama kinachochukia umasikini, chama kitakachoongoza na kutumia rasimali zetu nyingi kuendeleza watu wetu..

Ndio maana tumekaa kimya kuepusha mpasuko zaidi ndani ya chama katika kipindi hiki cha uchaguzi.

Hata hivyo katika wakati muafaka na mda sio mrefu nitazungumza na kutoa muelekeo wangu katika jambo hili kubwa.

Nimepata Jumbe nyingi, simu nyingi, nawahakikishia Watanzania na wanachadema kwamba nimewasikia na nitazungumza
.

Screenshot_20241221_095805_X.jpg
 
Wote walioshangilia kifo cha Magufuli laana iwatafune
 
Freeman kama ana akili akae pembeni...hapo ndipo historia itamkumbuka
Ni ngumu Sana hilo kutokea.
Viongozi wengi wa vyama vya upinzani ni mapandikizi ya Tiss.
Mfano ni Augustine Mrema, Cheyo, Lipumba, Mabere Marando, n.k
Wakuu,

Heche ameandika haya kwenye ukurasa wake wa X

Tuna jukumu la kihistoria la kuhakikisha tunaipatia Nchi yetu chama mbadala, na serikali mbadala itakayowatumikia watu na kuwaondoa katika umasikini wa miaka 63 ya Uhuru.

Serikali na chama kitachopinga rushwa bila aibu, chama kinachochukia umasikini, chama kitakachoongoza na kutumia rasimali zetu nyingi kuendeleza watu wetu..

Ndio maana tumekaa kimya kuepusha mpasuko zaidi ndani ya chama katika kipindi hiki cha uchaguzi.

Hata hivyo katika wakati muafaka na mda sio mrefu nitazungumza na kutoa muelekeo wangu katika jambo hili kubwa.

Nimepata Jumbe nyingi, simu nyingi, nawahakikishia Watanzania na wanachadema kwamba nimewasikia na nitazungumza
.

Sawa
 
Mwanzo nilijua kabisa CDM ni chama cha siasa,kumbe nilikuwa nā fikra za kikafili kudhani hivo .
Hiki chama ni cha familia nā kumweka mtu Mwngne lazma akubali mashariti ya familia ya waasisi akiwemo nā mkubwa .
Pole Heche nā Lissu.
Tumetoka sehemu Moja ila nakuomba toka CDM haraka tuanzishe chama chetu waasisi wawe wana Mara
 
Freeman hawezi kukaa pembeni kwa sababu kuna watu wametumwa kuiua CHADEMA !
Freeman amehangaika sana na CHADEMA kuliko huyo Lissu ! Freeman amekaa sana jela kwa ajili ya Demokrasia ya nchi hii.Sasa hawezi kutokea mtu eti akabeza alichofanya Freeman nchi hii.Mtu analeta tamaa na anasema uongo ili watu wamuonee huruma ! Huyo hafaiiii !
Wakati Freeman na wenzie wanahangaika nchi nzima kuikuza CHADEMA Lissu alikuwa Ughaibuni anachangisha pesa na haijulikani kazipeleka wapi ! Alipewa michango mingi sana ya matibabu hakuna aliemuuliza kaitumiaje lakini kwa tamaa yake aliporudi eti anaidai serikali impe stahiki zake ! Stahiki ni kwa yeye wakati ule kupata matibabu ambayo watu walishamchangia na akatibiwa ! walio ratibu masuala yote hayo ni CHADEMA wakiongozwa na mwamba Mbowe !
Kama aliwezeshwa akapata matibabu hizo anazotaka alipwe ni za nini ?? Anapeleka wapiiii ? Hii ni tamaa ! Kwa muktadha huo huyu Lissu anaonyesha kuwa ni mtu wa tamaa na hatufai kwenye uomgozi.Ukijumlisha na uongo anao zungumza vyote vinamuondoa katika sifa ya kuwa kiongozi wa chama na hata taifa huko baadae.
 
Back
Top Bottom