Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, John Heche, amesema kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Stephen Wasira ana haki ya kusinziaa kutokana na umri wake mkubwa na kuwataka wananchi wasipoteze muda kumjadili.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara mjini Bunda leo Jumatano Februari 12, 2025, Heche amemtaja Wasira kama destructor (mharibifu) na kudai kuwa ameletwa tena katika siasa ili kuwatia wananchi kwenye malumbano yasiyo na tija badala ya kushughulikia viongozi wakuu wa nchi.
Akinukuu maneno ya Hayati Bob Marley kutoka wimbo wake Rat Race, Heche alisema:
"In the abundance of water, the fool is thirsty" (Katika wingi wa maji, mpumbavu ana kiu).
Akitumia nukuu hiyo kueleza hali ya nchi, Heche amesema Tanzania ni taifa lenye utajiri mkubwa wa rasilimali, lakini wananchi wake bado ni masikini kutokana na uongozi mbovu na sera zinazoshindwa kuwanufaisha.
Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Ameeleza kuwa, madini ya Tanzanite yanayopatikana Tanzania pekee duniani yameweza kuajiri zaidi ya watu milioni mbili nchini India, huku Tanzania nzima ikiwa na wafanyakazi wa serikali wasiozidi laki tano.
Kwa mujibu wa Heche, Chama cha Mapinduzi (CCM) kimechoka na sasa kinafanya recycling ya viongozi waliopitwa na wakati.
Amesema kurejeshwa kwa Wasira katika siasa hakuwezi kuleta mabadiliko yoyote kwa sababu mfumo ule ule unazalisha matokeo yaleyale.
"Huwezi kutegemea kuokota kopo ukayeyusha ili utengeneze chuma, ni lazima litengeneze kopo vilevile," alisema Heche, akimaanisha kuwa viongozi walewale hawawezi kuleta suluhisho jipya kwa changamoto za nchi.
Aidha, amewataka wananchi kuamka na kuamua hatma yao kwa kuhakikisha watoto wao wanapata elimu na fursa bora badala ya kuendelea kurithi umasikini wa kutengenezwa na mfumo uliopo.