Hegemonic War: Urushwaji Angani wa Sputnik na Warusi, uliogofya sana Ulimwengu wa Magharibi:

Hegemonic War: Urushwaji Angani wa Sputnik na Warusi, uliogofya sana Ulimwengu wa Magharibi:

Mgambilwa ni mntu

JF-Expert Member
Joined
May 30, 2017
Posts
2,869
Reaction score
3,187
Wakiwa wanaelekea kumaliza WW II, mwaka 1945; Mataifa ya Allies yalianza kutofautiana juu ya namna ya kuiadhibu Ujerumani ya Hitler. Warusi na Wafaransa walitaka Ujerumani ifilisiwe kabisa ili iwe masikini lakini Marekani haikupendelea njia hiyo. In fact Marekani na Ulaya Magharibi waligundua kuwa, Urusi alitaka kueneza ukomunisti katika Mataifa ya Ulaya so wakaanza kutoelewana Hali iliyosababisha kushindwa kuiunganisha Ujerumani Magharibi (iliyokuwa chini ya USA, UK na France) vs Ujerumani Mashariki (iliyokuwa chini ya Urusi). Hali hiyo ilijitokeza pia kwa Korea baada ya kushindwa kuziunganisha Nchi za South Korea (Allies) vs North Korea (Urusi).
Adui mwenye nguvu katika WW II, alikuwa Mjerumani but katika hali ya kushangaza licha ya Ujerumani ku-surrender, Wajapan waliendeleza vita hasa maeneo ya baharini. Licha ya Japan kuonywa kusalimu amri ilikataa na kwa kuwa majeshi ya Allies yalikuwa yameshachoka kupigana Ulaya, Marekani iliyokuwa imegundua Bomu la Atomic, iliyarusha Mabomu hayo huko Hiroshima na Nagasaki na hivyo Wajapan wakakubali ku-surrender.
Wakati uhusiano umeshazorota kati ya Allies na Urusi, hasa jinsi walivyowatenda vibaya Wajerumani (Berlin Airlift), Warusi wakawa Taifa la pili duniani na la kwanza barani Ulaya kugundua Bomu la Atomic mwaka 1949 na kuwaogopesha Wazungu. Labda nayo iliharakisha uundwaji mwaka huo wa Umoja wao wa Kijeshi (NATO).
Mwaka 1952, USA waligundua Bomu la Hydrogen lakini katika namna ya kushangaza sana, Warusi walijibu ndani ya mwaka mmoja kwa kurusha Bomu la namna hiyo mwaka 1953.
Mwaka 1957, USSR ilifanikiwa kurusha Satelaiti (Sputnik 1) ya kwanza Angani (beyond the Earth's Atmosphere) na kuushangaza sana Ulimwengu, hasa Nchi za Ulaya Magharibi ambazo ziliogopa kuwa teknolojia hiyo imemfunika Mmarekani ambaye ndiye amekuwa msaada wao. In fact, Dunia nzima ilitambua kuwa ugunduzi huo wa Warusi umewapa upper hand dhidi ya Marekani kwenye masuala ya kijeshi na hivyo umehamisha Balance of Power towards USSR.
IMG_5344.jpg

Tena mwaka 1961, Warusi wakawa Taifa la kwanza kutuma Mwanaanga wao (Yuri Gagarin) angani (in the Space) na ambaye aliweza kuzunguka Mzingo wa Dunia.
Sputnik crisis - Wikipedia

Hata hivyo, kutokana na aibu ya Marekani kuzidiwa uwezo wa technolojia ya angani na Urusi, Rais wa Marekani aliamua kuji-commit mwaka 1961 kupeleka mwanaanga mwezini kabla ya Muongo haujaisha. Bahati nzuri walifanikiwa mwaka 1969, japokuwa damage ya kisaikolojia ilikuwa ilishafanywa tayari na Warusi kwao, hasa ukizingatia kuwa kiuchumi, Marekani ilikuwa ikiizidi mbali USSR.
IMG_5348.jpg
 
Leo hii watoto wa Dot Com hawawezi kuelewa ukubwa wa tishio la Urusi kwa Nchi za Magharibi lililokuwepo kati ya 1945 - 1989. Kutoka kuwa Taifa lililokaribia kusambaratishwa na Hitler 1939-41 huku likipoteza raia wengi zaidi kwenye WW II kuliko Mataifa yote, hadi kuwa Taifa lililoogopwa zaidi Dunia nzima.
Leo hii hakuna mtu anayeijua wala kuiheshimu Ukraine but I tell you, kwa kipindi hicho, USSR was synonymous to Russia and Ukraine, japokuwa zilikuwepo Nchi nyingi: Kazakhstan, Uzbekistan, Tadzhikistan, Azerbaijan, Georgia, Armenia, Latvia, Estonia, Belarus na Lithuania na Moldova.
Urusi iliposambaratika 1990, ilileta shida sana kwa kuwa mitambo mingi na viwanda vingi vya USSR, vilikuwa Ukraine. Ndiyo maana uhusiano wa Russia na Ukraine, ever since umekuwa mgumu.
 
Back
Top Bottom