Miti hii inauzwa pamoja na shamba Ina ukubwa wa hekta kumi+
Kuna miti iliyofikia umri wa kupasua au unaweza subiri miaka miwili
View attachment 2464333
Mkuu, ahsante kwa taarifa. Japo taarifa yako ina mapungufu ya msingi; hivyo siku nyingine jaribu kuongeza nyama kama ifuatavyo:
1. Aina ya miti (sawa umetaja)
2. Umri wa miti (haukutaja)
3. Ukubwa wa eneo (sawa umetaja)
4. Mahali shamba linakopatikana (Umetaja lakini ni too general, ungetaja kijiji, kata,a Wilaya na Mkoa)
5. Hati za umiliki wa eneo/ shamba (haujataja)
6. Gharama ( haukutaja, na hii ni muhimu sana)
7. Mawasiliano (haujaweka, kitu muhimu kabisa)
8. Sababu zilizopelekea kuuza (si muhimu ila ni vizuri kusema ili kuondoa wasiwasi, isijekuwa shamba lina mgogoro)
9. Msuala ya kitaalamu (mfano miti imepandwa kwa umbali gani kila mti, na je umewahi kufanya prunning au thinning?- Yaani umewahi kupunguzia matawi ya miti au kukata baadhi ya miti ili kuipa nafasi iote kwa ufasaha? Kama jibu ni ndio, ilikuwa mwaka gani na mara ngapi).
10. Je, ungependa mtu anunue shamba zima kwa mkupuo au hata mmoja mmoja anachukua kipande ni sawa?
Yote kwa yote, nikutakie mafanikio mema Mkuu.