Hekaya za George Soros na Utabiri wa Anguko la CCM

CCM mpaka sasa haipo isikuwa kuna polisi na tume fake
La kushangaza ni kuwa Chadema wakakaa na kuazimia kutumia rungu la pigo kuu la mwisho ambalo ni NO REFORM NO ELECTION lakini wanajitokeza watu tuliokuwa tunawaamini wanajiita G55 wanapinga matumizi ya hilo rungu ili turudi tulikotoka.
Hawa G55 hakika ni sawa na wale funza kama wale waingiao miguuni kule Kigoma. Hawa walikuwa FUNZA ndani ya Chadema na tulitembea nao.
Eti mtu unajua ukishiriki uchaguzi bila marekebisho muhimu ya sheria HAUWEZI KUTANGAZWA nawe unasema mie nitashiriki tuu! Hawa wakagombee huko TLP, UDP nk huku waondoke.
Hawa ni FUNZA55 tuu.
 
UnaUmMWa
 
Reforms wakati bunge limebakiza miezi michache lifikie tamati haitawezekana. Pia mmejipanga kisaikolojia kukubaliana na reforms zitakazofanywa na bunge ambalo zaidi ya 90% ni CCM? Au mtasusa tena? CHADEMA acheni kukurupuka. Ingieni kwenye uchaguzi mpate wabunge wengi watakaowasaidia bungeni. Vinginevyo mnachotaka kufanya ni uchokozi kwa dola.
 

Sio asilimia 90 ni zaidi ya 90%. Kumbe maamuzi ya bunge hili ni yale ya CCM sio ya wananchi?
Kuna kundi moja lipo ndani ya hiyo 10% iliyobaki mnalisahau kwa vile mnalifagilisha na kuzibua mitaro mnapo jisikia kuliamrisha, lakini hilo kundi lina nguvu kubwa ya maamuzi kuliko hiyo 90% mnayojivunia.
Eti muda hautoshi! Utatosha lini sasa? Nyie hamtaki uchaguzi huru na haki maboresho ya sheria yaweza kufanyika na kupelekwa bunge hili la bajeti ila hamtaki, sasa hautafanyika na yatakayo tokea ni yakubebwa nanyi migongoni mwenu.
 
Tajiri maelezo yako yamenyooka hayana konakona,weka namba kwa in bobo nikiuza ufuta uokote!
Hii nchi watawala wanatuona matako tu watu tulio chini.
Ukiwa unawasikiliza chadema unapata hali ya matumaini kwamba pengine kesho kutakucha.
Ukiwasikiliza kidumu chama kunawakati unahisi labda maendeleo waliyoyafanya ni huko mexco na sio hapa nchini,utasiiia tu nani kama mamaaa!

Kwa kweli labda ufuta uyeyuke,vinginevyo tajiri utaokota mapema tuuu!
 
Mkuu ulichoandika ndiyo uhalisia kwa 100% kama kuna mtu atabisha basi ni kutokana na upeo wake mdogo wa kuelewa mambo ila ukweli ni kuwa sasa hivi huu ni mwanzo wa mwisho wa CCM.
 
CCM hii inajimaliza yenyewe hivyo kufanya kazi ya vyama vingine kuwa nyepesi na ndiyo hoja ya mleta mada.
 
Wahenga walinena: "Sikio la kufa halisikii dawa!"
 
Hamna kitu! Ni chadema anayetaka kuichambua ccm
 
Kuna Mkoa mwingine baba ni Bilionea wa CCM na Serikali, mtoto ni Mwenyekiti wa Chipukizi.
 
Bandiko zuri. Mashaka yangu ni iwapo hao uliowaandikia kama watapata muda wa japo kuyafuatilia haya. Haishangazi kwani inawezekana ndio dalili za anguko lenyewe.
Mambo mawili umeyagusa ni muhimu sana.
1. CCM haiishi na uhalisia wa maisha ya wananchi wake.
CCM na serikali yake wanajaribu kuchora picha kuwa nchi iko vizuri kwa maana ya huduma kwa wananchi na wana uwezo wa kumudu gharama za maisha. Wamekuwa mabingwa wa kutaja takwimu bila kueleza ubora wa hizo takwimu. Haitoshi kuisjia kusema umejenga zahanati kila kijiji lakini hakuna watoa huduma, dawa au vifaa tiba. Na hata vikipatikana ni wangapi wenyebl uwezo wa kumudu.
Hali iko hivyo karibu kila sekta, changamoto ni kubwa lakini kwa sababu wanaishi tofauti na wananchi ndiyo inavyokuwa.

Ukitaka kuoiona hili vizuri angalia waziri na maafisa wa elimu wanaojinasuhu hali ni nzuri, watoto wao wanasoma wapi?
Jambo jingine ni vijana. Hili ni kundi ambalo limefanywa kuamini kwamba kazi ya kufikiri inapaswa kufanywa na aikina wassira. Jiulize kwanini siku hizi hakuna migomo? Je, vijana wanaridhishwa na hali iliyopo?
 
Concise documents....Hi nchi ina watu wenye upeo mkubwa sana , Moja wapo ni wewe:! Keep it up: haya nyie vilaza wa ccm ambao mnajua wazi mmepata nafasi ya kutuongoza kwa nguvu ya vyombo vya dola ;Tumieni hii kufanya reformism kabla ya anguko lenu ambalo hapo mbeleni lipo na mnajua.
 
Anguko la Ccm litaanza mwaka huu pale ambapo wapinzani watawaachia madaraka Ccm peke yao kitakachoenda kutokea ni straggle for the fittest na ule utimilifu wa maneno ya yule kiongozi wa Cdm wa kule Arusha
Namna nyepesi ya Ccm kuepuka kikombe hiki ni wao kuacha ubinafsi na kukubali kula na wenzao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…