mtwa mkulu
JF-Expert Member
- Sep 11, 2013
- 8,586
- 11,227
Wakuu heshima kwenu!
Ikiwa Leo ni siku muhimu kwa taifa letu;
Nimeamua kuwaandikia wale walio vijana sayansi ya kumudu kazi hii ya kizalendo.
Ni taaluma kama ilivyo taaluma nyingine za fizikia na uhandisi. Ukimaliza kusoma utakuwa na kiwango cha kutosha kuimudu kazi hii.
Ni kanuni ambazo ukimaliza kuzisoma na ukafuata kama nilivyo kuelekeza utaweza kulimudu jeshi la Tanzania na majeshi yoyote ulimwenguni.
Maisha ya dunia yamejengwa kwa misingi miwili, Imani na kanuni. Pasipo kuwa na haya dunia huenda mrama! Huwezi kufanikiwa.
Kwa kazi ya jeshi ni vyema kujua kanuni ambayo ipo katika sayansi hii unayoisoma.
Kuna kanuni Tatu, utachagua moja baada ya hapo maisha ya jeshi yatakuwa mteremko kama mlenda wa usangu! Amini ! Amini tuu utaweza! Hakuna jambo gumu lisilo na wepesi!
Hakuna bara bara ndefuu pasipo njia ya mkato labda tuu usiwe unaijua!
Hapo zamani hakukuwa na njia tatu kama sasa. Kulikuwa na njia moja tuu yaani KUGANGAMALA.
maisha ya jeshi ilikuwa kugangamala na si vinginevyo.
Kugangamala ni njia ambayo kwanza ukifika jeshini unatakiwa ulikubali jeshi. Usipo likubali unakuwa umefanya kosa kubwa sanaa lisilo rekebishika.
pili katika kugangamala ulitakiwa kukabiliana na kila kilichopo mbele yako. Ni rahisi! kila unacho ambiwa unafanya!
Kugangamala ilikuwa mbinu ya wengi walio fanikiwa hasa kwa kuwa maisha ya jeshi yalikuwa kama maisha ya nyumbani shida ni kuwa usicho kipenda nyumbani ndicho kilichofanyika Mara nyingi jeshini. Hapo unagangamala maisha yanakwenda!
Kwa sasa JKT wachache wanagangamala. hasa wale wanaotoka vijijini na wanafanikiwa!
Mbali na kugangamala kuna mbinu mbili zaidi hivi Leo ambazo wengi wamekili kufanikiwa Ya pili baada ya kugangamala ni KUJIONGEZA huku ya mwisho ikiwa ni KUJITOA UFAHAMU.
kujiongeza.
Ni namna nyingine ya kumudu mshindo wa jeshi.Utafiti unadurufu kuwa vijana kutoka mjini wanao jiunga na jeshi kwa shindikizo wamekuwa wakitumia mbinu hii. Kujiongeza ni msamiati ulio ingia Tanzania mwanzoni mwa mwaka 2014 ukimaanisha hali ya mtu kutenda kwa kiasi zaidi ya uwezo wako.
Kujiongeza jeshini kunahusisha kufanya jambo hata kama hupendi ama huwezi. Ukisikia jambo unatenda tuu kama ulikuwa huwez basi utaweza hauto kufa! Unaamini harafu unafanya.
kujiongeza kunahusisha mbinu zisizo za kawaida kama kujificha na kukimbia. Huku dada zetu wakiitoa hata miili yao! Huzuni wanajiongeza!
Angalizo mbinu hii si salama kwani ingawa vijana wengi wanaitumia ila katika vijana 100 ni sitini tuu walio fanikiwa kwa kujiongeza! wengi walishindwa kwa namna yoyote ikiwemo na kupata kumbukumbu na majeraha yasiyo sahaulika ama wawili watatu kupoteza maisha.
Vijana wa siku hizi wana mbinu ya mwisho ambayo watumiaji wake wengi wamefanikiwa!
Mbinu hii ni kujitoa ufahamu.
Namna ya kuifata njia hii salama na rahisi si kazi ngumu. Ukifika jeshini unajitoa ufahamu. Ikiwa ulikuwa Mtwa mkulu basi unatwaa nafsi nyingine.Unaweza ukafanya kwa namna mbili ama kuwa mnyama au kifaa. Ndio! unajipa hisia za Tembo au Nyumbu au kiboko na kuhakikishia hata pata kuwepo mkubwa zaidi yako jeshini. Unaweza kuwa Ngiri ama duma hakika hata kuwepo mkali zaidi yako jeshini! Unaweza kuwa punda pia hakuna zito utakalo libeba jeshini! Unaamini kisha unaanza maisha yako rahisi ya jeshini.
Unaweza pia kutwaa hisia za vifaa. vya chuma kama vile sururu hata nondo na Carter pillar! Utakuwa umejijengea maisha rahisi jeshini.
Katika mbinu hizo tatu umkumbuke MUNGU nahakika atakuongoza na kukupitisha kila hatua.
Ni sayansi yenye kanuni tatu; kanuni kama Althmetic na Pythagoras!! Zitumie na utakuwa shuhuda wangu. mzuri kwa maisha ya jeshini!!!
Utekelezaji mwema!!