Hekima aliyoomba Mfalme Suleimani

Hekima aliyoomba Mfalme Suleimani

Metronidazole 400mg

JF-Expert Member
Joined
Aug 25, 2016
Posts
941
Reaction score
2,062
Wengi wetu leo hii ukimwambia unataka Mungu akupe nini atakwambia pesa/utajiri.

Hata ibada nyingi kwenye haya makanisa binafsi ya mitume na manabii maombi makubwa ni Pesa! Mali! Utajiri.

Mfalme Suleiman alipoulizwa na Mungu anataka nini! Mfalme Suleiman akamwomba Mungu ampe hekima.

Hili si jambo dogo hata kidogo! Hakuomba Mali aliomba Hekima.

Mungu alishangazwa mno na hili pengine hakutegemea, akampa hekima aliyoomba lakini zaidi aamuongezea na utajiri mali na ukuu.

Mpaka leo hii hakuna mtu anayefikia utajiri aliokuwa nao mfalme Suleiman.

Lakini Bwana Mungu hakuishia hapo, akaona mali zote hizi na hekima aliyoomba, havitamfaa kitu kama hatapata ridhiko la matamanio ya kimwili.

Akaona amuongezee mvuto na nguvu za kumiliki wake wa ndoa mia saba (700) na Masuria (nyumba ndogo) mia tatu (300).

Acheni Mungu aitwe Mungu akitaka kukupa hukupa vyote, Mia 7 kwa mia 3.

Tafakari matendo ya Mungu kwa hekima kuu.
IMG_20241124_113945.jpg
 
2 Mambo ya Nyakati 1:7-12.

Agano la kale, Old testament
 
Ni Moja ya Hadithi katika hadithi au masimulizi mengi ya Biblia.

Ukwasi wa bwana Solomon, na Mambo kibao yanakuzwa mno.

Achilia mbali wanazuoni wa biblia ambao wengi wao baadhi ya Hadithi na masimulizi ya Biblia yanatupiliwa mbalii na hayana ushahidi wa kihistoria, archeology & anthropology.

Mfano wa wanazuoni hao ni akina Richard Elliot Friedman, Israel Frankenstein, Neill Asher, Williams g Dever, James l kugel.

Si kila fiction Haina mafunzo na maarifa, zinginee fictions zipo vzrr mno.

Lakini nzuri ukiwa na utambuzi wa kuwa hii ni fiction na hii non fictions.
 
Back
Top Bottom