Dunia inatangaziwa kutatokea mafuriko baada ya siku tano.
Dalai Lama anawaambia waumini wa kibudha inatakiwa wafanye tahajudi (meditation) na wasubiri kuzaliwa upya (reincarnation).
Papa anawaambia waumini wa kikatoliki duniani kutubu dhambi zao na kuomba.
Lakini, mwalimu wa kiyahudi (Rabbi) anawatangazia wayahudi wote wana siku tano za kujifunza kuishi ndani ya maji.
Uwezekano wako wa kufanikiwa hautegemei elimu, dini yako, rangi yako, kabila, uzoefu wako wa zamani au jinsia bali hekima uliyoipata wakati wa kujifunza. Hata biblia inasema katika kitabu cha Mithali 14:24 “Taji ya mwenye hekima ni mali zao; Bali upumbavu wa wajinga ni upumbavu tu”.
Tunamsoma mfalme Sulemani alijua vyema kanuni za maisha na ndio maana hakujisimbua kuanza kuomba utajiri, alijua akiomba hekima utajiri utamfuata tu. Na ndio maana mwanafalsafa mmarekani Robert Nozick (1938-2002) amewahi kusema “hekima ndiyo unayohitaji ili uishi vizuri na kutatua matatizo pamoja na kuzuia hatari katika mazingira uliyopo”.
Siri ya utajiri inajulikana sana vyema na wayahudi. Pamoja na kwamba karibu kila mtu anaamini wayahudi ndio watu waliobarikiwa zaidi na Mungu na wenye akili sana kuliko kila mtu duniani. Ukweli ni kwamba wayahudi wanajua siri ya kufanikiwa na ni kanuni ya dunia mwenye mafanikio huheshimiwa zaidi.
Sasa kama wanaongoza kila nyanja kwanini tusiwaheshimu. Najua unajua ya kwamba hata kama Mo Dewji au Bill Gates akikueleza alikopitia kuwa tajiri hautaweza kupita katika njia zake zaidi utahamasika wakati unamsikiliza na baada ya hapo kesho jua kali likikupiga utaanza kulaani hata kwanini upo duniani.
Myahudi na mwanafizikia Albert Einstein anasema “hekima sio zao la kwenda shule na kusoma mambo mengi bali uzoefu wa maisha katika kusudi la kuitafuta hekima”
Ni kwa namna gani tunaweza kupata hekima?. Hekima inapatikana kwa kuwa mnyenyekevu, kusoma vitabu na kukutana na watu wengine. UNYENYEKEVU ndio kitu cha msingi zaidi katika safari ya kupata hekima kama Mithali 11:2 inavyosema “kijapo kiburi ndipo ijapo aibu bali hekima hukaa na WANYENYEKEVU”.
Unapokuwa mnyenyekevu inaonesha utayari wako kujifunza mambo mengi zaidi ya unayojua. Unapokuwa mnyenyekevu unaonesha kwamba wewe si mtaalamu na upo tayari kujifunza kutoka kwa kila mtu. Siku zote watu wanyenyekevu ni watu wenye kufundishika, wenye uwezo wa kubadilika na zaidi hawaachi kujifunza.
Kuna usemi kwamba ukitaka kuficha pesa mtu mweusi asione basi weka katikati ya kitabu. Sipingani na huo usemi kwani watu wengi weusi hasa watanzania wenzangu ni wavivu sana kusoma. Je nikikwambia sehemu nyingine ya kupata hekima ni kusoma vitabu?. NDIO, kusoma vitabu, tafiti iliyofanyika Uingereza na Marekani ilionesha wayahudi wana uwezo mkubwa wa akili kuliko wengine.
Wayahudi ni watu wenye kupenda kujua kwa namna gani kitu fulani kinatokea na wafanye nini kukabiliana nacho. Muda mwingi kabla hata ya kuanza kutafuta mali wayahudi hutumia kusoma vitabu, vikiwemo vya dini ya kwao na vingine vyenye kubeba maarifa ya dunia. Wayahudi wanathamini sana vitabu na hata vikiharibika huwa wanazika kwa ajili ya kutoa heshima na si kutupa kama tufanyavyo wengi wetu.
Mwanafalsafa mwingine wa kiyahudi Samuel Ibn Tibbon anasisitiza “fanya vitabu rafiki zako”. Kama haitoshi Zig Ziglar anasema “watu masikini wana runinga kubwa na maktaba ndogo na watu matajiri wana runinga ndogo na maktaba kubwa”. Binafsi naenda kinyume kidogo na Zig kwani watu wetu wengi masikini wana runinga kubwa na hawana vitabu kabisa bali CD za filamu mbalimbali na flash zenye nyimbo za kusumbulia wengine akichomeka kwenye radio kubwa ili kusumbua majirani. Basi katika vitabu kuna maarifa mengi, maarifa mengi yanaongeza hekima na hekima inaleta utajiri.
Ninaelewa tuna imani tofauti za dini lakini hekima na utajiri haihitaji kujua dini yako ni ipi. Kila mwenye mafanikio huheshimiwa na watu wa kila imani, wasomi na wasio soma. Mafanikio yana uhusiano mkubwa sana na namna tunvyofikiri na hapo ndipo hekima hufanya kazi yake.
Buddha anasema “akili yako ndio kila kitu, unavyowaza ndivyo unavyokuwa”. Mwandishi Henry David Thoreau anakazia “kile mtu anachojiwazia zaidi ndicho kinachotengeneza hatima yake”. Ni kawaida wengine kuona pesa kama chanzo cha uovu, hasa kama imani zetu zifundishavyo. Lakini ukweli ni kwamba pesa sio shetani bali inategemeana na nani anatumia na kwa njia gani. Inashauriwa KUWAPENDA WATU NA KUTUMIA PESA.
Wanaowapenda watu hupata pesa na mali kwa ajili ya kuendelea kuwasaidia watu. Pesa huleta tiba ya kuishi mazingira mazuri, kuvaa nguo nzuri na kupata chakula kizuri. Tatizo huja pesa ikipendwa zaidi ya kitu chochote kile. Umasikini husababisha watu kuendelea kulaani na hata kufanya matukio ya uharifu.
Kama anavyosema Kiyosaki badala ya kufanya kazi ili upate hela uifanye hela ikufanyie kazi ni ukweli tupu. Naelewa vyema utauliza je kama sina hela ya kunifanyia kazi? Jibu ni rahisi, fanya kazi kwa mwaka mmoja hadi mitano kisha tumia hiyo hela ikufanyie kazi. Kufanya kazi kila siku ili kupata hela huo ni UTUMWA WA PESA. Unapata muda mwingi wa kujifunza na kusoma unapokuwa na hela tayari kuliko usipokuwa nayo kwani muda mwingi utatumia kuitafuta.
Na hiyo ndiyo sababu ya mwalimu wa kiyahudi Elezar ben Azariah kusema “ pasipokuwa na hela hakuna kujifunza”. Anaendelea kusema “kama watu hawajala wakashiba na kurizika hawawezi kujifunza, kukua kiroho na kufanya kazi vizuri”. Wenye hekima na pesa hupenda kuendelea kuwa na pesa ili kusaidia wengine na kuwajali. Kitabu cha kiyahudi ‘Talmud’ kinaandika “umasikini ukiwepo nyumbani unazidi magonjwa hamsini”. Na tena Talmud inamwona mtu masikini kama mtu aliyekufa kwani hawawezi kujisaidia mwenyewe wala wengine.
Tumeshaona kufanikiwa unahitahi hekima na kisha kutengeneza akili yako kuwa chanya na kuwa na imani. Na jambo lingine ni kufanya kazi. Ndio KUFANYA KAZI. Nakubaliana na hayati Magufuli “HAPA KAZI TU”, ndio hata Mithali 12:24 inasema “mkono wa mwenye bidii utatawala bali mvivu atalipishwa kodi”.
Wayahudi wengi wanajifanyia kazi zao na kuajiri wengine badala ya kuajiriwa. Na wameweka uwekezaji katika sekta nyeti wao wakiwa kama waanzilishi na wakurugenzi watendaji. Pia huamini binadamu ni watengenezaji na si watumiaji. Mungu alimuumba mtu kwa mfano wake hivyo mtu ni mwumbaji au mtengenezaji wa vitu hapa duniani.
Unapofanya kazi basi lazima kutengeneza malengo na kutia juhudi katika kufanikisha hayo malengo. Ukifanya kazi kwa umakini ndani ya saa moja ni tofauti na kufanya kazi kwa zaidi ya masaa manne bila umakini.
Leonard Bernstein ambaye ni myahudi anayeishi marekani anasema “kufanikisha mambo makubwa unahitaji mambo mawili; kuwa na mpango na kisha kutumia muda vizuri. Andika malengo au yaweke akilini kisha elewa hatua za kuchukua na uzifanyie kazi”. Unapokuwa na malengo hakikisha yanaeleweka na kisha tia umakini (focus) katika malengo. Furaha huja kwa kutimiza malengo.
Kufeli kusikufanye kutofikia malengo na mafanikio. Kwani mtu akipotea njia si hurudi na kutafuta njia sahihi? Na mtu akidondoka si hunyanyuka? Basi uvumilivu wakati wa kazi ni muhimu, hakikisha haupotei njia ya kile unachotaka maishani. Penda unachofanya na utaona matokeo yake. Fanya kazi kwa muda na tunza kidogo unachopata na wekeza baadae. Panda mti wa pesa kwa ajili ya watoto wako. Usidharau kuwekeza kidogo chako hata kidogo. “shilingi mia moja unayoweka akiba ni bora kuliko elfu moja unayotumia”.
Kati ya kosa ambalo hautakiwi pia kulifanya ni kuhakikisha kuwa hauwekezi katika jambo usilolijua na haujalifanyia utafiti. Fanya utafiti kwa nguvu zote, tafuta washauri wa uwekezaji/uchumi. Wengi wamefeli katika kuwekeza kwa sababu ya kutumia mawazo yao na jeuri.
Mhubiri 11:2 inatufundisha kwamba inatakiwa tugawanye uwekezaji katika sehemu saba au nane kwani hatujui ni wapi tutapata hasara. Kuwekeza katika kitu kimoja na kutegemea hichohicho kinaweza kutuumiza sana tukipata hasara kuliko kugawanya uwekezaji.
Mfano mzuri ni Bhakresa group au Mo. Wote wamewekeza katika vyanzo mbalimbali. Hata wakipata hasara sehemu moja watanufaika na sehemu nyingine.
Let us vote now! Ahsanteni!

Upvote
4