HEKIMA YA JIONI: Mtazamo Wako ndio Unaamua Ugumu au Urahisi wa Kitu

j'cob mushi

Member
Joined
Feb 26, 2013
Posts
21
Reaction score
13
Mtazamo ni vile ambavyo mtu amejengewa au amejijengea maana fulani au imani fulani juu ya jambo fulani. Mtazamo waweza kutengenezwa kutokana na mazingira unayoishi vitu unavyosoma, kutazama na kufuatilia. Mtazamo pia unaweza kutengenezwa na aina ya watu unaojihusisha nao kila siku.

Mfano unakaa na watu ambao wanasema hawawezi kuuza bidhaa kwa kumfata mtu na kunwelezea faida za bidhaa. Lazima utajikuta na wewe unaanza kuiga na kubadilisha mtazamo wako hasa kama ulikuwa huamini hivyo.

Unakaa na watu ambao wanapenda kulalamika na kuona ugumu kwenye kila jambo lazima utajikuta unaanza kufanana nao kimtazamo.

Mtazamo wako juu ya mambo unayopitia ndio unaamua wewe uwe kwenye hali gani.
Unaweza kukuta watu wawili wanapitia hali ngumu zinazofanana halafu mmoja ana furaha kama kawaida huku mwingine akilalamika kila wakati.

Watu wengi wanalalamika hawana mtaji wa kuanzia biashara lakini si kweli hawana. Mtaji wanao ila walishajiambia kwamba kazi fulani siwezi kuifanya kabisa.
Siwezi kuuza kwa namna hii.

Badili mtazamo wako ili uweze kuona uwezekano kwenye kila hali unayopitia.
Mtazamo wako ndio unashape maisha yako.


Ni mimi Rafiki Yako,
JacoMushi.

Piga Hatua Timiza Ndoto Yako
USIISHIE NJIANI
 
Last edited by a moderator:
Habari Rafiki, Leo ni siku nyingine tena ambayo tumepewa kama zawadi kwa ajili ya kwenda kuyafanya Maisha yetu yawe bora Zaidi.

Jisemeshe Maneno Haya Kabla Hujatoka Kwenda kufanya Chochote.

“NACHUKUA HATUA, NAJIFUNZA, NAWEKA JUHUDI NA BIDII, NAVUMILIA.
MAFANIKIO NI HAKI YANGU, EEH MUNGU NIWEZESHE.”

Kwenye mtihani shuleni tulikuwa tunaambiwa yale maswali ambayo unayaweza ndio unatakiwa uyafanye mapema sana kabla akili haijachoka, yale magumu ndio utayafanya baada ya kumaliza yale ambayo una uhakika nayo.

Ukitumia nguvu nyingi kwenye yale ambayo uwezo wako ni mdogo unakuwa unajipa nafasi ya kukata tamaa mapema na hata kushindwa kufanya yale ambayo una uwezo wa kufanya.
Daudi alipomwona Goliathi hakuangalia sehemu nyingi alizojiziba na chuma kwa haraka haraka macho yake yalimpeleka kwenye paji la uso lililokuwa wazi hivyo na yeye akalenga palepale.

Walikuwepo mafundi wa kurusha mishale pale vitani lakini hakuna alietazama paji la uso lililokuwa wazi wote walikuwa wanatazama yale manguo ya chuma aliyovaa. Wote walitazama kifuani palipojaa chuma wakasahau kwamba mshale ungeweza pia kupita kwenye paji la uso.

Wewe tatizo lako unatazama mambo makubwa kumbe ili uweze kutimiza haya makubwa ungefanya jambo moja dogo tu ambalo ulikuwa unalidharau au kuliona halina matokeo makubwa.

Yale mambo magumu kwenye Maisha yako ambayo huwezi kuyabadili nikiwa na maana kwamba yapo nje ya uwezo wako kwa wakati huo, inakupasa ukubali ukweli huo kisha usonge mbele katika kutazama kile ambacho una uwezo nacho.

Tafuta kidogo chenye manufaa, endelea kutafakari ni wapi ambapo ukisema uchukue Hatua utakuwa ndio mwanzo wa wewe kuelekea kufanya yale makubwa unayoyataka.

Ni mimi Rafiki Yako, Jacob Mushi
[HASHTAG]#UsiishieNjiani[/HASHTAG]
“Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.”
VITABU
 
Last edited by a moderator:
kweli mkuu unakazana ununue trecta au pumpu kubwa ya 5,000,000 ya kumwagilia ndo uanze kilimo wakati unaweza kuanza na haa pump ya 400,000
 
Habari Rafiki,

Leo ni siku nyingine tena ambayo tumepewa kama zawadi kwa ajili ya kwenda kuyafanya maisha yetu yawe bora zaidi.

Jisemeshe maneno haya kabla hujatoka kwenda kufanya chochote.

“NACHUKUA HATUA, NAJIFUNZA, NAWEKA JUHUDI NA BIDII, NAVUMILIA.
MAFANIKIO NI HAKI YANGU, EEH MUNGU NIWEZESHE.”

Mojawapo ya watu ambao wanaishi kwa mateso duniani na huzuni ya ndani kwa ndani ni wale ambao wanafanya vitu ili kuwaridhisha wengine.

Unavaa mtindo fulani ili umvumtie mtu fulani akupende, ndugu yangu kama hujaajiriwa na shirika la kijasusi basi unajitesa bure.

Unabadili kabisa mtindo wa maisha yako ili tu umvumtie mtu fulani au uendane na aina ya watu fulani.

Ukijikuta unaacha kuwa wewe na kuanza kubadilika kuwa mtu mwingine ujue unajipoteza. Ipo siku utakuja kuona ulikuwa unapoteza muda bure.
Hao unaotaka kuwavutia siku wakigundua sura yako halisi watakukimbia.

Unachopaswa kufanya ni kuhakikisha unakuwa wewe na unajiongeza uwe bora kila siku. Watu sahihi wataambatana na wewe.
Waache watu wakupende vile ulivyo maana hutapata shida kufanya vitu vya ziada ili upendwe.

Ishi maisha yako vile ambavyo unapata furaha hata ukiwa mwenyewe watu sahihi watakuja kwako.


Ni mimi Rafiki Yako, Jacob Mushi
“Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.”
 
Habari Rafiki, Leo ni siku nyingine tena ambayo tumepewa kama zawadi kwa ajili ya kwenda kuyafanya Maisha yetu yawe bora Zaidi.

Jisemeshe Maneno Haya Kabla Hujatoka Kwenda kufanya Chochote.

“NACHUKUA HATUA, NAJIFUNZA, NAWEKA JUHUDI NA BIDII, NAVUMILIA.
MAFANIKIO NI HAKI YANGU, EEH MUNGU NIWEZESHE.”

Mambo mengine yanakuwa magumu kwasababu mtazamo wako unavuta ugumu. Inakupasa kutengeneza mtazamo wa kushinda kwenye yale mambo unayofanya.

Mtazamo wa kushindwa ndio unawakwamisha watu wengi na kuwafanya waogope kujaribu. Mtu anaanza kuona kushindwa ndani yake kabla hajachukua hatua yeyote.

Wapo watu ambao wanaweza Kukutengenezea mtazamo wa kishindi na kushindwa. Watu hawa ni wale ambao umewaamini sana na kuwapa nafasi ya kuwasikiliza.
Wakisema jambo fulani haliwezekani hata kama ulikuwa una hamasa kubwa kiasi gani unajikuta umekubali kushuka chini na kuwasikiliza.

Kaa na watu ambao wanakutia moyo na kukueleza ukweli, watu ambao wameshajaribu mambo makubwa zaidi yako. Ukikaa na watu ambao hawajawahi kufanya chochote kikubwa yaani wewe kwao ndio umefanya makubwa zaidi utajikuta wanakukatisha tamaa.

Marafiki waliokwisha kufanya makubwa zaidi yako watakuambia jambo fulani usifanye hivi fanya hivi na wala hawatakukatisha tamaa. Wanaweza wakakwambia hili usifanye sasa hivi anza na hili kwanza. Hivyo unapaswa kuwaelewa pia pale wanapokupa ushauri.

Tengeneza mtazamo wa kushinda ili uweze kupambana na changamoto unazopitia kila siku.

Ni mimi Rafiki Yako, Jacob Mushi
[HASHTAG]#UsiishieNjiani[/HASHTAG]
“Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.”
VITABU
 
Last edited by a moderator:
[HASHTAG]#HEKIMA[/HASHTAG] YA LEO : Ushindi Mdogo ni Ushindi Mkubwa.

Usidharau Kile kidogo unachokifanya. Daudi alijua kwamba anaweza kumpiga Goliath baada ya kutazama kule alipokuwa. Kujaribu kwake kupambana na dubu kulimpa nguvu kwamba hata Goliath si kitu mbele yake.

Ushindi mdogo mdogo unaopata kila siku ndio unakuonesha kuwa unaweza kufanya makubwa zaidi.

Ni ngumu kuamini unaweza linapokuja jambo kubwa, kama hujawahi kufanya jambo dogo ukapata ushindi.

Hapo hapo ulipo sasa hivi kuna vitu unaweza kuvifanya weka nguvu zako zote. Weka uwezo wako wote. Ipo siku utatumia hivyo vitu kama njia ya kupata makubwa zaidi

Jacob Mushi
[HASHTAG]#usiishienjiani[/HASHTAG]
 
Last edited by a moderator:
#Ni kweli Maisha hayajawahi kuwa marahisi ila kuna sehemu unaweza kuwa unazidisha ugumu wewe mwenyewe.

“Pale ambapo wewe ni Mjinga Ndipo Wengine Wanakufaidi”


#Ni kweli huwezi kujua kila kitu na ndio maana kwa vile vitu ambavyo huvijui lazima ulipie gharama za kujua. Bahati mbaya sana wengi tunashindwa kutambua ni vitu gani hasa tunavihitaji na kujikuta tunakazana kutafuta vile ambavyo wala hatuvihitaji sana.


#Ni hatari sana kama unamiliki simu ya milioni 3 halafu huna biashara yeyote unayomiliki. Au kama sio biashara basi huna kipato ambacho kinazidi bei ya simu yako kwa mwezi. Sio vibaya kumiliki simu ya ghali ubaya upo pale ambapo wewe unalalamika hali ngumu Maisha hayafai na mengine ya ajabu.


[HASHTAG]#Inashangaza[/HASHTAG] kumkuta kijana anapenda udaku kuliko mambo yenye maana yeye muda wote yupo bize na habari ambazo hakuna kinachoongezeka kwenye Maisha yake. Lazima Maisha yawe magumu kama hujaupa ubongo wako kazi ya kufikiri. Kama hujaamua kujishughulisha na mambo yanayoongeza thamani yako lazima utaongeza ugumu wa Maisha yako mwenyewe.


#Ni kawaida sana ya watu kupenda vitu virahisi bahati mbaya ni kwamba ukitaka Maisha yako yawe magumu chagua kufanya vitu virahisi. Yale magumu unayoacha ndio unayafanya yatengenezee Maisha yako ugumu Zaidi.


[HASHTAG]#Lile[/HASHTAG] usilolifahamu ndio unalilipia gharama. Maisha yako yataendelea kuwa magumu Zaidi kama utakataa kujifunza na kuendelea kubeza watu wanaofanya kazi ya kufundisha na kuandaa semina na kwa ajili yako.


[HASHTAG]#Usikubali[/HASHTAG] kuyafanya Maisha yako yawe magumu Zaidi. Ni vizuri ukajua kwa sasa wakati unapambana ni vitu gani ni vya muhimu Zaidi na vingine ni anasa. Anasa ni vile vitu ambavyo hujafikia uwezo wa kumiliki lakini wewe ukakimbilia kumiliki. Kukopa pesa na kununua gari hiyo ni anasa, kumiliki biashara inayokuingizia kipato na kikakutosha ukajinunulia gari lako haiwezi kuwa anasa.


[HASHTAG]#kama[/HASHTAG] huna vipaumbele lazima Maisha yako Yazidi kuwa magumu. Kama huna ratiba ya Maisha yako lazima uzidishe ugumu kwenye Maisha. Kama huna utaratibu wa Maisha lazima ugumu uongezeke. Jua ni vitu gani umevisababisha wewe na vile ambavyo huwa vipo siku zote.


Ni mimi Rafiki Yako, Jacob Mushi

[HASHTAG]#UsiishieNjiani[/HASHTAG]

“Chukua Hatua, Timiza Ndoto Yako.”
 
Last edited by a moderator:
Umezunguka sana mjomba kumbe ujumbe uko mwisho kabisa.nimekupata shukran
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…