Hekma na busara

sicu

Member
Joined
Dec 31, 2012
Posts
69
Reaction score
22
Kwanini wanaume wenye hekma na busara mumeoa walio baki masharobaro na waaribifu, wauza unga, wavuta bangi, na tulio taka tusubiri tukomae kwanza, kumbe tulikataa bahati.
Niliona ktk movie jamaa mmoja akisema "unapiga mateke bahati wewe", nikawaza wengi tulipiga mateke bahati hivi eh?.
Ndio mipango ya mungu kila mtu na rizk yake. Wa moja ni wa moja. Bahati haiji mara 2, waswahili walisema.
So nimebakia kuongea ongea na kujipa moyo, na kujijibu mwenyewe, hahaha. Kuna kaka mmoja wa kichaga aliniambia wewe ni nsuri sana, wanawake wasuri matatizo, nikaona duh,
Mwengine wa kingoni akasema yeye anataka miguru baja,
Mwengine wa kisukuma akasema ananiogopa sababu ni nzuri,
Mwengine wa Kizenji akasema mwanamke mwenye elim na pesa mjeuri, nikaona duh,
ukiwa nzuri matatizo, ukiwa na elim matatizo ukiwa na pesa matatizo, ukiwa masikini matatizo ukiwa kama tofari matatizo, haya jamani
Bora niende kijijini nikaolewe na kibabu mkulima, maisha wawili wawili, kufa kuzikana na maisha popote penye upendo na amani, mambo ya PHD yamenishinda, Good luck 2 all.
 
Ha ha ha haaaa!! Pole saana but kumbuka kila kitu hupangwa na Allah, hao wote sio waliopangwa kuwa nao that while, mambo ya Elimu, pesa na sura yalishapitaga kitambo saaana!! Alafu niombe/tuombe radhi sio wote ambao hatujaoa ni wahuni, wauza unga, waaribifu but ni hatujapata machaguo yetu kutoka kwa mungu, Mfano mimi binafsi naish mwenyewe na natamani na kuhitaji kuwa na mwenza but Bado hajatokea(sijampata) sasa nitaoa vip kama nakutana na vicheche tu??

pesa, uzur na elimu sio vikwazo vya Mapenzi kwenye mapenzi ya kweli !! Elimu haina dhamani katika mapenzi ina dhamani katka maisha tu!!
 
mbona unanitisha mwnzngu mana kuna mkaka nimemkatalia masuala ya kunioa mpk na mm nipate kazi mana nimetoka kmliza chuo iv karibuni iv kumbe nikikosa kabisa ntamkumbuka
 
mbona unanitisha mwnzngu mana kuna mkaka nimemkatalia masuala ya kunioa mpk na mm nipate kazi mana nimetoka kmliza chuo iv karibuni iv kumbe nikikosa kabisa ntamkumbuka

Woga wako ndo umasikini wako, tafakari chukua hatua!!
 

Sawa, lakini naamini ukiwa na hivo vitu unatatizo kubwa maishani ya kupata mume. so matatizo ya mwanamme kutopata mke hata siyajui,
 
mbona unanitisha mwnzngu mana kuna mkaka nimemkatalia masuala ya kunioa mpk na mm nipate kazi mana nimetoka kmliza chuo iv karibuni iv kumbe nikikosa kabisa ntamkumbuka

Nami nilifanyaga hivo hivo, ila sasa naona nilipiga bahati mateke.
Kuna kipindi watatokea wengi kutaka kukuoa utawakataa kwa sababu unazojua wewe,
ukiwa teyari kutaka kuolewa mmmmm, watatokea wavuta mangi wauza unga, utaona kama mungu kakulaani jamani, so my experience ndio hiyo my sis
 
duuh naogopaje mwenzio but naamini mungu mwema endlea tu kumuomba my ccta
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…