Mpekuzi Tanzania
JF-Expert Member
- Mar 11, 2018
- 650
- 1,016
Nimepita Igunga nikielekea Muleba kwa ajili ya Mwaka Mpya na Familia yangu. Nimesimama kwenye Kituo cha mafuta kinaitwa Galaxy hapo Igunga, Kuna tatizo la vyoo nilikuwa naliona maeneo mengi ila jamaa wameweza. Vyoo visafi husikii harufu ya mikojo wala kinyesi. Maji vyooni ya kutosha na sabuni za kunawia kwenye masinki ni uhakika. Watanzania tujifunze biashara zinahitaji uwekezaji na sio kujaribu. Heri ya Mwaka Mpya.