Heko Kaone sanaa group

lulu za uru

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2015
Posts
2,557
Reaction score
3,221
Sikutegemea kama kuna siku ningekaa na kufuatilia tamthiliya ya kiswahili ya kibongo tangu kuvunjika Kaole sanaa group,Enzi zile marehem mpendwa wetu kanumba akiwa hajaota kitambi,Ray akiwa hajajichubua!...ohh siku zile za marehem mzee kipara,Pwagu na wengine wengi....Hakika kaole imerudi kama kaone sanaa group ungana nao tv1 saa mbili kamili usiku halafu utanirudishia feedback...tamthilia inaakisi maisha halis ambayo watanzania weng wanaishi kwa sasa,visa vya mama mkwe,ndoa za mitala,michepuko nk..mimi ningekuwa naandaa tuzo za filamu abadan nusu ya tunzo ingeishia kaone ..they are so pure..hawafoji! anayenipinga anyooshe mkono..natabiria kina kanumba wengi kuzaliwa ktk hiki kikundi
 

safi sana!..hiyo saa mbili ni kila siku?..hawana marudio weekend?
Mi nlikuwa nampendaga sana yule aliyekuwa anaact kama Mama Kibakuli!..nae yumo?
 
Mama Kibakuli yupo na yule mke mwingine wa Muhogo Mchungu pia yupo, wote wanaigiza kama wake wa Muhogo Mchungu. Marudio itakuwa Jumapili, leo niliona kwenye mudabkama wa saa saba mchana.
 
wala haikuwa lengo la kutangaza tunashare tu mawazo ili tufurahie maisha..
 
Mama Kibakuli yupo na yule mke mwingine wa Muhogo Mchungu pia yupo, wote wanaigiza kama wake wa Muhogo Mchungu. Marudio itakuwa Jumapili, leo niliona kwenye mudabkama wa saa saba mchana.

hahahahahahaha...Bi Staa!.,kuna filamu nilimuona kapatapata supu kanoga!
Tatizo vipaji tembo,kipato sisimizi!
Cc: chige kwa ufafanuzi!
 
Last edited by a moderator:
hahahahahahaha...Bi Staa!.,kuna filamu nilimuona kapatapata supu kanoga!
Tatizo vipaji tembo,kipato sisimizi!
Cc: chige kwa ufafanuzi!
Upiversity,

Nimefuatilia huo mjadala manake nami nilitamani sana nishuhudie hiyo kitu lakini naona lulu za uru hajaweka ratiba kamilibut nitafuatilia! Nitafuatilia coz' mimi ni mpenzi sana wa tamthilia... tena sana! Hata zile za Hollywood; mie naangalia sana series kuliko movie na jinsi nilivyo na passion ya tamthilia, nakumbuka wakati TV1 inaanzishwa nilijaribu kutaka kupeleka tv pilot halafu wao wafanye wanayobaki coz' bado naamini Tanzania tuna waigizaji wazuri sana; kinachokosekana ni stori! Kwa bahati mbaya mambo yakaingiliana nikashindwa ku-move on na idea yangu!
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…