Heko Shukuru Kawamba, Mwaka jana Bongo Fleva Mwaka huu matusi ya nguoni!

Ngandema Bwila

JF-Expert Member
Joined
Sep 8, 2010
Posts
1,017
Reaction score
258
Sasa inabidi nianze kuwapongeza watumishi wa serikali wanaofanya madudu katika kazi zao kwa sababu wamekuwa SUGU, hawasiki wala kuona aibu wakilaumiwa au kulalamikiwa kwa utendaji wao mbovu. Leo nimemshuhudia Kwamba akitangaza bila soni kufuta matokeo ya wanafunzi 700 kwa kuandika matusi kwenye answers sheets zao. Mwakajana mwanafunzi mmoja aliandika mistari ya bongo fleva, mwaka huu matusi baado waziri yumo tuu.

Naamini matokeo haya ni mbinu ya viongozi wetu kuwaandaa watoto wao kuwa watawala na watoto wetu watawaliwa wa milele.
 
Kawambwa hongera kwa upumbavu uliotukuka
 

Watoto wa chadema hao wenye matusi
 
Hongera sana kwa mitaala maalumu toka kwa nyambari nyangwine.
 
Sasa wakubwa kwa hali hii mpaka mwanafunzi anakuwa na hasira na ubovu wa system anaamua kutukana kwenye karatasi yake ya mtihani basi Tanzania imekwisha.
Mbatia aliomba mitaala iletwe bungeni mavuvuzela wakapuliza mavuvu sasa yametokea.
Wakina nape watakuja na hoja kuwa hawa wanafunzi wazazi wao ni chadema.

Hatua za haraka zinahitajika la sivyo ule mtaji wa wajinga utaongezeka

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Hapa bwana Kiwete inabidi uweke mbali undugu huyu jamaa wako Dr Kawambwa habebeki yeye pamoja na wasidizi wake wanapaswa kuondoka! kutoka 32% mwaka 2011 mpaka 54% mwaka 2012! :-* nadhani hapa maji mazito kuliko damu...ila nina uhakika hili suala litakuwa twisted kuwa ni Dr Kawambwa anaondolewa kwa vile Muislam kama kawaida ila ikumbukwe alipokuwa waziri wa Miundombinu alifanya madudu pia akahamishwa wizara elimu hajakaa hata muda tayari madudu mengine! Nina uhakika kuna viongozi wa Kiislam wanaofanya majukumu yao ipasavyo kama Prof Makame Mbarawa ila huyu Dr Kawambwa nina uhakika ni undugu wa karibu na Mh Rais ndo unambakisha pale
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…