HEKO TFF

Rio Tinto

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2014
Posts
777
Reaction score
451
Sisi binadamu ni viumbe wa ajabu sana, wagumu kuelewa, wepesi kusahau. Pia ni wepesi kulaumu mambo yanapokwenda ndivyo sivyo lakini wagumu kupongeza pale mambo yanapoenda vizuri.

Leo nataka niwe tofauti na wengine kwa kutambua mafanikio ya uongozi wa sasa wa TFF chini ya Ndugu Wallace Karia.

Haya ni baadhi ya mafanikio ya uongozi wa sasa wa TFF.

1. Uteuzi wa mchezaji bora wa Afrika mwaka 1994 Emmanuel Amunike kuwa kocha mkuu wa Taifa Stars. Safari yetu ya AFCON ilianzia kwa maamuzi haya ya TFF. Wengi tuliponda sana uteuzi huo lakini sasa wote tunacheka na kufurahi.

2. Kuendesha Ligi kuu TPL bila mdhamini kwa msimu mzima huku mipango ikiendelea kuhakikisha mdhamini anayepatikana ananufaisha klabu shiriki kama zinavyonufaika na TV sponsorship ya Azam TV. Habari chini ya kapeti kuna mazungomzo yanayoendelea na mdhamini kutoka South Africa.

3. Kuwezesha kufanyika kwa mkutano wa FIFA hapa nchini uliohudhuriwa na viongozi wakuu wa soka duniani akiwemo Raisi wa FIFA Giani Infantino na Raisi wa CAF Ahmad Ahmad. Viongozi hao wawili walipata fursa ya kukutana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

4. Kuwezesha kurudishwa kwa fedha za maendeleo ya mpira kutoka FIFA zilizositishwa kutokana na matumizi mabaya ya fedha chini ya uongozi uliopita. Kutokana na kuridhishwa na uwazi pamoja na uwendeshaji wa shughuli za TFF chini ya uongozi mpya, FIFA itatoa TZS 11.5 Billion kwa ajili ya maendeleo ya mpira nchini.

5. Kuwezesha Taifa Stars kufuzu AFCON 2019 kwa mara kwanza baada ya miaka 39 ya kutoshiriki mashindano hayo makubwa barani Afrika. Hakika historia itawakumbuka.

6. Kuwezesha Tanzania kuandaa mashindano ya AFCON kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17

7. Kujenga taasisi imara, ni dhahiri shahiri kwa sasa TFF kama taasisi ipo stable na imara chini ya uongozi wa Wallace Karia pamoja na changamoto kutoka kwa wale waliojaribu kuleta migogoro hapo kwenye shirikisho. Tunashukuru Jamhuri iliwachukulia hatua wale waliojaribu kuleta migogoro isiyo na manufaa.


Mungu aendelee kuwabariki viongozi wetu wa TFF chini ya Ndugu Wallace Karia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
watu wanaleta uyanga na usimba lakini jamaa anajitahidi mno, na mambo yake yanaleta mafanikio.. ule mchezo wa kukalia kupiga mishe za hela umeisha. wengi wao kandambili wanasingizia eti jamaa ndo anaingiza matatizo kwenye soka wanasahau kwamba matatizo yapo ndani ya timu yao ambayo haina uongozi madhubuti. Mi nampongeza pia kwa maamuzi yake ya kuongeza idadi ya wachezaji wa kulipwa kutoka watano hadi kumi. hii inasaidia vijana wetu wa ndani kujifunza mbinu za uchezaji wa mpira na kujiamini, mfano mzuri ni sasahivi mafanikio ya simba pia yanaonyesha njia na kuongeza hamasa kwa timu ya taifa nayo imeanza kufanikiwa. wanaomsema mabaya Karia tumeshawazoea wao kila mahali ni kuongelea mapungufu tu kuhusu mafanikio ya mtu hawataki. Na hawa wanaopinga sana kwenye soka ukiwachunguza ndo wale wale wanaopinga hata kwenye siasa na ndo haohao wanapinga hata ushindi wa stazi kwamba eti kabahatisha., na ndo haohao wanapinga uchaguzi yanga usifanyike....KARIA we ongoza baba mungu atakusaidia mafanikio yako yanaonekana.
 
Wewe ni Kandambili(Yanga)??

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndio tatizo la washabiki wa mpira wa Tanzania ni hili la usimba na uyanga. Mtu anatoa hoja ya msingi halafu unauliza kama kandambili au yeboyebo. Wewe kama unafatilia mpira wa miguu duniani, je uliwahi kuona wapi timu ikicheza michezo ya raundi ya pili wakati ana rundo la michezo ya raundi ya kwanza hajacheza? Tusilete mahaba kwa vile mapungufu hayo yana mbeba Simba au Yanga. Ratiba ipo vuluvulu timu zingine zimecheza mechi 31, zingine 30, zingine 29, wengine 28 na nyingine 21 na pia ligi yetu mbovu.



Sent using Jamii Forums mobile app
 

Unaweza kuainisha ni matatizo yapi hayo ambayo kandambili wanadai kuwa yameletwa na TFF ili tuone ni uongozi wa kandambili au ni TFF ndio tatizo.

Hivi ili Taifa lifanikiwe tunahitaji wachezaji wengi kutoka nje waje wacheze Tanzania au tunahitaji watanzania wengi watoke nje wakacheze mpira wa kulipwa?




Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…