Heko Utumishi, ila maombi ya kuhama kupitia kwa waajiri, ni pigo kubwa sana kwa watumishi

Heko Utumishi, ila maombi ya kuhama kupitia kwa waajiri, ni pigo kubwa sana kwa watumishi

Mikhail Tal

JF-Expert Member
Joined
May 12, 2016
Posts
421
Reaction score
778
Ni kuhusu hii taarifa ya utumishi kuruhusu watumishi kufuata wenza wao wa ndoa. Kwanza niwapongeze utumishi kuliona hili kwamba ni tatizo ndani ya utumishi, familia nyingi na ndoa zimeparanganyika kwasababu ya haya maamuzi ya kumpangia kazi mtumishi mbali na familia na mwenza wake.

Ila sasa, kuna tatizo lingine linajitokeza, Katibu Mkuu Utumishi alitoa barua ya watumishi kutuma maombi yao ya kuhama kupitia kwa waajiri wao ambao wata process na kutuma majina utumishi.

Binafsi kabisa, nimekosa amani na huu mfumo wa maombi kupitia kwa waajiri, na hii ni kutokana na suala kwamba kuna wafanyakazi wa halmashauri kama walimu na kada za afya ambao wameanza kufanyiziwa mtima nyongo pale wanapopeleka barua zao na maombi.

Kwanza zoezi limejeuka, too much manual process, watu wanaambia waandike barua waweke mpaka address saba na kibaya zaidi kuna taarifa hata waliopeleka maombi kwenye baadhi ya halmashauri, maombi yao yametupwa kapuni, kwa ahadi ya 'Tutashughulikia'.

Tunaomba wizara na katibu mkuu utumishi waangilie hili suala kwa kina, ingependeza sana kama mfumo wa ESS ungetumika ingekuwa bora sana kuliko hizi tikitaka zinaendelea Halmashauri.
 
Ni kuhusu hii taarifa ya utumishi kuruhusu watumishi kufuata wenza wao wa ndoa. Kwanza niwapongeze utumishi kuliona hili kwamba ni tatizo ndani ya utumishi, familia nyingi na ndoa zimeparanganyika kwasababu ya haya maamuzi ya kumpangia kazi mtumishi mbali na familia na mwenza wake...
Mdogo wangu aliomba uhamisho Toka Tanga mwaka wa nne Sasa kimya!
 
Back
Top Bottom