Heko Wakenya

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Posts
94,296
Reaction score
122,540
Heko kwa uongozi wa juu wa serikali ya Kenya (rais na makamu wake), heko kwa viongozi wa bunge na bunge zima, heko kwa Law Society of Kenya, na heko kwa civil society at large kwa kukemea kwa nguvu zote upumbavu, ukiukwaji wa haki za kibinadamu, na muhimu zaidi uhalifu dhidi ya wanawake kwa kisingizio eti cha kulinda maadili (kama vile huo uhalifu waufanyao ni maadili!!!).

Rais kakemea, makamu wake Bw. Ruto naye alikemea, Aden Duale kakemea na Law Society of Kenya imeomba ruhusa maalum kutoka kwa mkurugenzi wa mashitaka ya kuwashitaki wanaume wanaowavua wanawake nguo hadharani kwa kisingizio cha kulinda maadili.

Natamani na Tanzania tungekuwa hivyo lakini nasikitika kusema kuwa kwenye jamii yetu bado idadi ya watu wajinga ni kubwa mno.

LSK seeks to prosecute men stripping women

Nairobi, Kenya: The Law Society of Kenya (LSK) has sought special permission from the Director of Public Prosecution to prosecute men stripping women in public.

The LSK Chairman Mr. Eric Mutua said that the National Police Service should also immediately form a special unit to patrol areas where the crimes are likely to happen.

“The ongoing brutality that is stripping our women in public for allegedly dressing in an indecent manner must be brought to an end,” Mr. Mutua said.

The LSK Chairman said that there are criminal elements within the Kenyan male population that has also taken to defiling, assaulting and insulting women by stripping them naked.
Mr. Mutua said that video clips of women being stripped naked have gone viral on Facebook and Twitter handles, which must be contained.

“These kinds of actions are not only illegal but immoral by all standards and should never be tolerated or condoned in a civilized society,” Mr. Mutua said.

The LSK Chairman said that the professional body is petitioning the office of the Director of Public Prosecution (DPP) Mr. Keriako Tobiko for special permission to prosecute the criminals.

“LSK wants to be granted special leave by the DPP to prosecute any person arrested in connection with stripping, defiling or insulting women in public,” Mr. Mutua said.
He said that the National Police Service should also form a special unit to assist the public in apprehending the suspects.

Mr. Mutua said that any member of the public has a civil duty to arrest any person who commits or is likely to commit an offence.

“Any man or woman who witnesses any person molesting, defiling or stripping a woman should arrest and deliver them to the nearest police station/post,” Mr. Mutua said.

Hundreds of protestors took to Nairobi streets recently to condemn the humiliating public stripping of three women.
The mobilisation for the protest started through the social media under the hash tag #MyDressMyChoice .
The protestors marched from Uhuru Park to a bus stage on Accra Road where people alleged to be touts were earlier filmed ripping off a woman’s clothes for allegedly dressing indecently.
 
Last edited by a moderator:
hiyo sheria ije tanzania haswa vijana wa kariakoo wanahitaji kuwajibishwa kwa upuuzi wao wa kudhalilisha wanawake
 
hiyo sheria ije tanzania haswa vijana wa kariakoo wanahitaji kuwajibishwa kwa upuuzi wao wa kudhalilisha wanawake

Wapuuzi, wanafiki, washenzi wakubwa hao.

Kwanza hawana maadili yoyote yale.

Mtu mwenye maadili mema hawezi kumvua na/au kumchania mtu mwingine nguo zake, iwe hadharani au faraghani kisa tu hajapenda mavazi ya huyo mtu mwingine.
 
Nilishawahi kuandika hapa, Uhuru Kenyatta utendaji wake wa kazi kama Rais wa Kenya unanivutia na hata watendaji wake wa chini pia labda wanaanza kumuiga Boss wao au wenzetu wameweka kipaumbele cha kusimamia maslahi ya Kenya na Wakenya kwa kila hali. Tanzania tunaona wizi mkubwa wa pesa, hazina hakuna pesa, mahospitali hakuna madawa, Rais wa nchi kauchuna utadhani hayamhusu. Saa zote yeye ni kiguu na njia.
 
dah kama ule udhalilishaji aliyefanyiwa yule dada kwa kosa la kuiba dera........ilisikitisha sana......
 
His exellence ni Vasco da Gama in the new world

Btw anatafuta misaada

Aibu naona mimi kuwa Mtz

Tatizo kupata green card ni kisanga!
 
Reactions: BAK
nadhani nyerere aliwahi sana kutupatia uhuru.....angeacha kidogo wakoloni watushape ubongo kama nchi nyingine ilivyokuwa.......haswa katika maswala ya utawala na usimamizi wa hazina ya nchi katika kuleta maendeleo........
 
Ni sawa lakini iwekwe pia sheria ya maadili kuhusu hao wanaotembea karibia uchi! Mtu anavaa nguo inabakiza cm mbili chupi kuonekana si ukosefu wa maadili pia. Si vema kuwavua lakin sheria iangalie kotekote
 
Sheria ya mavazi mtu awapo mtaani akijifanyia mambo yake?

Unaumwa wewe!
 
Wapuuzi, wanafiki, washenzi wakubwa hao.

Kwanza hawana maadili yoyote yale.

Mtu mwenye maadili mema hawezi kumvua na/au kumchania mtu mwingine nguo zake, iwe hadharani au faraghani kisa tu hajapenda mavazi ya huyo mtu mwingine.

umeona eeeh nashangaaga hawa vijana sijui wamelelewa wapi? sasa ukishanchania akabaki uch* then ndo maadili gani hayo ila yote hiii ni kukosa kazi tu
 
dah kama ule udhalilishaji aliyefanyiwa yule dada kwa kosa la kuiba dera........ilisikitisha sana......

uliona ile video hivi iliishaje ile issue yule dada aliaibika sana
 
Wapuuzi, wanafiki, washenzi wakubwa hao.

Kwanza hawana maadili yoyote yale.

Mtu mwenye maadili mema hawezi kumvua na/au kumchania mtu mwingine nguo zake, iwe hadharani au faraghani kisa tu hajapenda mavazi ya huyo mtu mwingine.

Kariakoo mnavuliwa mkiiba, na pia jifunzen kuvaa kutokana na mazingira huwez enda kariakoo na kimin utadhan unaenda club...
 
Africa imejaa unafiki sana. Mijanaume iko busy kufisadi pesa za umma wasiposhikwa wanakula raha maisha yote, na wala hakuna anayewafanya kitu. Lakini wao ndio wa kwanza kutoa hukumu za kijinga barabarani - mbona kuna makabila hadi leo wanatembea manyonyo nje? Hata kule Igunga wapo, huo ndio utamaduni halisi wa mwafrika - nguo zililetwa na wazungu baadae sana kabla mwafrika hawajawahi kufikiri kama kuna uwezekano wa kuufunika mwili kwa nguo - zaidi ya kutembea uchi au kusitiri baadhi ya viungo tu kwa magome ya miti au majani, leo miafrika ndio inayojifanya utamaduni kuvaa nguo ni wao - unafiki mtupu - shame upon all who do this - stop violence against women
 
Kariakoo mnavuliwa mkiiba, na pia jifunzen kuvaa kutokana na mazingira huwez enda kariakoo na kimin utadhan unaenda club...

Kwa nini usiweze? Hiyo marufuku imeandikwa wapi?

Attitudes kama zako ndo huwapa hamasa hao wahuni kufanya uhalifu wao.
 
Sheria ya mavazi mtu awapo mtaani akijifanyia mambo yake?

Unaumwa wewe!

say whatever lakin hzi nguo ambazo znaonyesha karibu na chupi hazifai kutembelea mtaani. Unamwonyesha nani uch wako kwan kuna mtu hana uchi? Sisapoti kuwavua hadharani lakini kuna haja ya wao kubadilika pia
 
Mtu anayefikiria kwa upeo mkubwa na kufanyia kazi mambo ya maana hatakaa akawaza mwana fulani kavaa nguo fulani na kwa sababu fulani, there's no sound mind that can do that. Wanaofanya hivo ni opposite.
 
say whatever lakin hzi nguo ambazo znaonyesha karibu na chupi hazifai kutembelea mtaani. Unamwonyesha nani uch wako kwan kuna mtu hana uchi? Sisapoti kuwavua hadharani lakini kuna haja ya wao kubadilika pia

Chupi siyo uchi!

Kuvaa mini skirt si sawa na mtu kutembea uchi.

Acheni kutia chumvi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…