Hela ni nyoko.... Ukiwa nazo hata wazazi wanakutetemekea.... Sembuse demu?

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,107
Reaction score
160,001
Binti mmoja alitoroka kijijini kwao na kukimbilia mjini kutafuta maisha, akarudi kwao baada ya miaka mitano. Na muda wote huo alikuwa kimya hakuandika barua wala kutuma ujumbe.

Siku hiyo ghafla akarudi kijijini akiwa kwenye gari jipya zuri sana. Mtu wa kwanza kukutana alikuwa baba yake ambaye wakati huo alikuwa anatoka kilabuni kunywa pombe.

Ile kumtambua tu binti yake ambaye wakati huo kajichubua ngozi na kuwa mweupe Fulani hivi, kavaa nywele bandia, kope bandia, na jino la dhahabu bandia, mzee akamcheki kisha akaanza kumpa vipande vyake ‘We mwanaharamu umeondoka hapa kwa miaka mitano na hukutaka kutuandikia barua wala kutuma salamu, unajua ulimtesa sana mama yako?’ Binti akajiumauma kisha akamjibu baba yake,’ Baba unajua niliona niwe kimya maana kazi niliyokuwa nikifanya msingefurahia’.
Baba yake akauliza ‘Kwani ulikuwa unafanya kazi gani hiyo ambayo tusingeifurahia na wewe ndiye binti yetu?’

Binti akajibu huku anaangalia chini, ‘Baba nilikuwa nafanya kazi ya umalaya’. Duhh mzee akawa mbogo mara dufu, ‘Unasema nini we mwendawazimu? Yaani ulikuwa huko mjini unalitia nuksi jina la ukoo wetu na kijiji chetu? Nakuambia hivi, geuka sasa hivi urudi ulikotoka, mimi ntainuaje uso wangu hapa kijijini, watu wakijua hiyo kazi uliyokuwa unafanya mjini?’

Binti akamwambia baba yake, ‘Sawa baba ntaondoka ila kuna zawadi nimeleta naomba niziache. Nimemletea mama sanduku la nguo na kanga 20 na pesa kidogo milioni tatu. Na wewe baba nimekununulia hili gari nililokuja nalo na nimekufungulia akaunti ina milioni kumi, na ntakuwa naongeza kila mwaka ili isipungue, utaweza kupumzika kulima sasa, na ntakujengea nyumba nyingine ya kisasa’

Mzee alikuwa kama kapigwa shoti, pombe yote ikamtoka akabaki mdomo wazi anamwangalia tu binti yake. Akili ilipomrudia akamuuliza binti yake, ’Mwanangu mpenzi samahani, ulisema ulikuwa unafanya kazi gani mjini?’ Binti akajibu ‘Samahani baba nilisema kuwa nilikuwa nafanya kazi ya umalaya’. Mzee akachekaa saana na kusema, ‘Unajua sikukusikia vizuri ndio maana nilikasirika. Eti nilisikia umesema ulikuwa unafanya kazi ya uyaya, ndio nikakasirika na kusema binti yangu mzuri kwanini umekubali kufanya kazi ya kulea mtoto wa mtu? Karibu nyumbani mwanangu mpenzi’
 
Mzee wangu japo mimi nilikuja kuonana nae ukubwan kabisa nakuhakikishia asingepokea chochote na andekutoa baru. Yule dingi japo alikuja kuwa mshikaji wangu sana nikimuangalia hana tofauti sana na Magufuli. Ni wale wazee wakuda Promax. Mkuria flan kwake hela hakuwa nazo za kiivyo ila haendeshwi na hela kabisa. Kwake muhim ni simu kila baada ya siku mbili basi. Na akikuhtaji uende
 
Back
Top Bottom