SoC04 Hela ya kujikimu kwa wanachuo itolowe kila mwezi badala ya kila baada ya miezi 2

SoC04 Hela ya kujikimu kwa wanachuo itolowe kila mwezi badala ya kila baada ya miezi 2

Tanzania Tuitakayo competition threads

The Student

New Member
Joined
May 30, 2024
Posts
3
Reaction score
1
Wanafunzi wengi wanapojiunga na Elimu ya Juu wamekuwa wakinufaika na ada, ela ya kujikimu, utafiti n.k. inayotolewa na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu ili kuweza kuwawezesha kukamilisha masomo yao.

Napenda kuipongeza Serkali kwa kuongeza kiwango cha ela ya kujikimu kufikia shilingi 10000/= kwa siku, kwani hii imepelekea wanafunzi wanufaika kuweza kumudu baadhi ya maitaji yao.

Utaratibu ambao umekuwa ukitumika katika kutoa ela ya kujikimu kwa wanufaika umekuwa ni kutoa kwa awamu mbili ndani ya muhula mmoja kiasi kiasi cha Shilingi Laki Sita (600,000/=) kila nusu muhula ambayo kwa jumula mnufaika hupata kiasi cha shilling millioni moja na laki mbili kwa muhula mmoja (1,200,000/=). Vivyo hivyo Muhula wa pili mwanafunzi mnufaika hupata kiasi cha shilingi 1,200,000/= kwa mhula wa pili. Hivyo basi kwa mwaka wa masomo ambao ni mihula miwili sawa na miezi 8 mwanafunzi hupokea kiasi cha shilingi milioni mbili na laki nne (2,400,000/=).

Kwa utaratibu huu wa sasa, huwa inachukua Zaidi ya siku sitini au zaidi kwa mwanafunzi mnufaika kupata tena ela ya kujikimu kutok Bodi ya mikopo ya elimu ya juu.

Utaratibu huu umekuwa na changamoto sana kwa wanufaika Kutoka na hali hii ya kusubiri kwa kipindi cha miezi miwili kupata tena ela ya kujikimu, wanafunzi wengi wamejikuta wakipata shida mbalimbali katika kutimiza mahitaji yao mhimu kwani muda uliopo kati ya siku ya kupokea adi kupokea kwa awamu nyingine ni miezi miwili ambacho ni kipindi kirefu kwa mwanafunzi anayetegemea iyo ela kuendesha masomo yake kwa kila kitu.

Hali hii imepelekea maisha ya baadhi ya wanafunzi kuwa magumu sana hasa kipindi cha mwezi wa mwisho wakiwa wamesubili kupokea ela ya kujikimu kutoka Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu. Ndani ya muda uo wanafunzi wengi wamekuwa wakiingia kwenye madeni ili waweze kukidhi mahitaji yao ata wanapopokea ela huwa asilimia kubwa inaishia kwenye kulipa madeni.

Wengine hukosa kabisa chakula na kuanza kuwa tegemezi, wanafunzi wengine hujikuta wakipata mulo mmoja kwa siku hali inayodholotesha afya zao na utendaji wao.

Kutokana na muda wa kupokea ela yua kujikimu kuwa mrefu wanafunzi wanaoishi kwenye nyumba za kupanga wamekuwa wakiingia kwenye migogoro na wamiliki wa nyumba wanazopanga na kupelekea wengine kufukuzwa.

Na muda mwingine wanafunzi wamekuwa wakikosa ela ya kutumia kwenye kazi zinazotolewa Vyuoni na kupelekea kushindwa kufanya na kuwasilisha kazi zao ndani ya muda uliopangwa. Zaidi wanufaika wengine wanaoishi mbali na vyuo wanavyosoma wamekuwa wakikosa nauli ya kufika chuoni na kupelekea kutohudhuria kikamilifu darasani na kupelekea kupata changamoto kwenye matokeo yao.

Changamoto zote hizo zimekuwa zikitokea kutoka na muda uliowekwa wa kupokea ela ya kujikimu kuwa mrefu sana. Hivyo basi ili kuweza kunusuru taaluma za wanafunzi wanufaika wa ela ya kujikimu kutoka bodi ya mikopo ;

Napendekeza ela ya kujikimu kwa wanufaika kulipwa kila mwezi kuanzia mwezi wa kwanza wa muhula wa kwanza adi mwezi wa mwisho wa muhula wa pili.

Mwaka wa masomo ni mihula miwili ambayo nio sawa na miezi 8 hivyo basi badala ya kutoa kiasi cha shilingi shilingi laki 6 kila baada ya miezi 2 ni bora zaidi mwanafunzi kupokea kiasi cha shilingi laki tatu (300000/=) kila mwezi kuanzia mwezi wa kwanza manzoni mwa muhula wa Kwanza ambao ni November adi mwezi wa mwisho wa muhula wa pili. Hii itasaidia Zaidi;

1. Mwanafunzi kuweza kutatua changamoto zinazojitokeza kwa dharura. Kuna matukio mengi huwapata wanafunzi kama magonjwa,ajari , na wengine wamekuwa na matatizo ya kiafya tangu zamani, mwanafunzi anaweza kutatua changamoto inayomkabili ndani ya muda kuliko kupata shida na kusubili ela inayotolewa baada ya muda wa miezi 2, inayotolewa wakati ata akiba aliyoiweka imeshaisha na amelimbikiza madeni.

2. Kupunguza shida wanazopitia wanafunzi wakiwa wamesubili ela ya awamu nyingine ambayo inatoka baada ya miezi 2 Ambayo inapelekea baadhi ya wanafunzi (sio wote) kujiingiza kwenye vitendo hatarishi ili waweze kupata mahitaji yao. Mwanafuzni atakapopata ela ya kujikimu itakuwa rahisi kwake kufanya maamuzi sahihi ya ela aliyoipokea.

3. Mwanafunzi ataweza kupanga bajeti yake ya mwezi mzima kwa kutenga ela ya chakula. matumizi ya shule , nauli n.k. kutokana kwamba ela ya kujikimu huwakuta tayari washajiingiza kwenye madeni basi itakuwa musaada sana kama ela ya kujikimu itatolewa kila mwezi. Hii itawasaidia sana wanafunzi wanaopanga panga vyumba kwani anaweza kutenda bajeti yake na kuweza kuhakikisha analipia chumba chake ndani ya muda husika na kuepusha migogo ambayo huwa inawaathiri kisaikolojia.

kama inawezekana kwa watumishi wa Serkali na sekta binafisi kulipwa kwa mwezi ili waweze kutimiza mahitaji yao au bajeti ya mwezi mzima bila kulimbikiziwa mshahara . Basi itafaa zaidi kwa wanafunzi wa vyuo vikuu kupokea ela ya kujikimu ambayo itakuwa laki tatu (300,000/=) kila mwezi badala ya kulimbikiziwa na kupewa baada ya miezi miwili au zaidi. Hii tawasaidia sana kufikia malengo maana e;la inayotolewa kila baada ya miezi miwili huwa wengi hawanufaiki nayo wanaishia kulipa madeni waliyokopa wakati wakisubilia ela nyingine.

Mwisho, napenda kushauli Taasisi mbalimbali zinazohusika kuweza kuondoa changamoto ambazo zinapelekea wanafunzi wanuifaika kushindwa kupata ela ya kujikimu ndani ya muda mwafaka kwani wanafunzi wengi wanategemea ela ya kujikimu kuendesha maisha yao, inapocheleweshwa ata kwa siku moja inakuwa changamoto kwa wanufaika kufikia malengo.
 
Upvote 1
Changamoto zote hizo zimekuwa zikitokea kutoka na muda uliowekwa wa kupokea ela ya kujikimu kuwa mrefu sana. Hivyo basi ili kuweza kunusuru taaluma za wanafunzi wanufaika wa ela ya kujikimu kutoka bodi ya mikopo ;
Umeeleza changamoto nyingi sana, lakini pia hatuoni kama vyuoni ndiyo mazingira bora sana kwa hao wanafunziwatuwazima kujifunza kujisimamia na kujipangia bajeti wenyewe?

Tukiwalea na kuwalinda hadi umri huo ni lini watajifunza kwa vitendo? Je hawataishia kuwa wateja wa kausha damu waililie tena serikali mara alfu? Kuna faida ya kuyapata matokeo ya maamuzi yako hapohapo (immediate feedback)

Mwisho, napenda kushauli Taasisi mbalimbali zinazohusika kuweza kuondoa changamoto ambazo zinapelekea wanafunzi wanuifaika kushindwa kupata ela ya kujikimu ndani ya muda mwafaka
Sahihi kabisa. Kwa wakati nuafaka uliokubaliwa. Kama ni mwezi kweli kila mwezi tarehe hiyo. Na kama ni miezi miwili basi iwe kila miezi tarehe hizohizo
 
Back
Top Bottom