Mwanzo walikuwa wanatuambia makusanyo ya kila mwezi, wakatuambia na matumizi yake potelea mbali hata kama walitudanganya, ajabu siku hizi naona kimya hakuna taarifa yoyote kuhusu hili suala.
Wanachotufanyia kwa sasa ni wizi, wanatuibia pesa zetu wanazitumia vile wanavyotaka wao, hapa naona kabisa kuna haja ya kwenda mahakamani kuwadai pesa zetu hawa wezi.