Helikopta kutua Mlima Kilimanjaro

Helikopta kutua Mlima Kilimanjaro

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826

1668439551327.png

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imesema imeridhishwa na miundombinu ya utalii ikiwemo viwanja vya kutua helikopta katika Hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro (KINAPA).

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Ally Juma Makoa amepongeza Wizara kwa kuboresha miundombinu katika eneo la Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro akisisitiza “sasa tunaweza kupanda mlima kwa urahisi.”

Makoa amesema Kamati imeridhika na utekelezaji wa miradi hiyo na kumshukuru Rais Samia Suhulu Hassan kwa kuendelea kuipatia fedha Wizara ya Maliasili na Utalii.

Kuhusu eneo lililokuwa linaungua kwa moto, Makoa amewathibitishia wananchi kuwa moto huo ulishadhibitiwa na Mlima Kilimanjaro kwa sasa ni eneo salama sana na shughuli za utalii zinaendelea kama kawaida.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja amesema: “Njia hizi mwanzoni zilikuwa zinaleta usumbufu sana na zilikua zinapelekea hata wale wageni wanaopata matatizo ya kiafya wakiwa mlimani, kuchelewa kufikishwa kwenye maeneo ya huduma mjini, lakini kwa sasa wanaweza kupatiwa huduma ya usafiri kwa haraka na kwa urahisi.”
 
Mruhusu sasa na vile vigari vinavyoendeshwa na umeme! Vinaitwa cable nini sijui! ili na sisi wengine tuje kutalii kwenye huo Mlima. Mambo ya kulazimishana kupanda kwa miguu hayakubaliki hata kidogo.

Nyakati fulani Waziri wa Utalii wa wakati huo Mh. Hamis Kigwangala alikuja na wazo la hivyo vigari vya angani, mlimpinga mwanzo mwisho! Kwa kisingizio eti wapagazi watakosa ajira, kana kwamba hakuna kazi myingine wanayo imudu katika maidha yao, isipokuwa hiyo tu ya kubebba mizigo ya Wazungu.
 
Utamudu hizo gharama?

Unajua madhara yake kwa nchi wanazotumia huo mfumo?
 
Nilipoangalia hiyo picha nikajua hicho kiwanja kiko juu ya mlima,sasa nashangaa naona kuna magari yamepaki mita chahche kutokea hapo,au magari siku hizi yanapanda mpaka juu...
 
Ndiyo unatakiwa utaje sasa hizo gharama, na pia hayo madhara ya kutumia huo mfumo. Kumbuka hii ni jamii forums
Madhara yake ni kupata magonjwa ya moyo, maana unatoka low elevation kwenda high elevation within a short time. Hivyo mwili utashindwa ku adapt mazingira ya kileleni hata kama utarejea starting point kwenye low elevations
 
Ally Juma Makoa ...... “sasa tunaweza kupanda mlima kwa urahisi.”
Adventure sio kufika Kilele cha Mlima Kilimanjaro kwa Helcopter,
Adventure ni kupanda mlima na kufika kileleni kwa nguvu zako!
Dhana ya kwamba kiwanja kimewekwa kwa ajili ya kurahisiha upandaji ni potofu!
 
Back
Top Bottom