Poleni wafiwa wote. KIfo cha Deo Filikunjombe ni pigo kubwa si kwa Ludewa pekee wala CCM, bali ni kwa Taifa zima. Deo alijipambanua kama mwanasiasa kijana aliyeweka mbele maslahi ya nchi, tofauti na wanasiasa wengine ambao kwao vyama ni zaidi ya nchi. Mara ya mwisho tulionana na kuaungumza na Deo katika hoteli ya St, Gasper, Dodoma. Hatuna la kufanya isipokuwa kumshukuru Mungu kwa kila jambo.