TANZIA Helikopta yaanguka, aliyekuwa Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe na wengine wapoteza maisha!

wema wafa mapema wabaya mbona hamdanjiiiiiiiiiiiiii???????
 
Deo ni kati ya wanasiasa waliofanya bunge lililomaliza muda wake kuonekana kuwa bunge la kisasa

Ni mbunge ambaye kwake nyeusi ni nyeusi
na nyeupe ni nyeupe bila kujali msimamo wa chama chake

Ni mbunge ambaye wananchi wa ludewa na taifa kwa ujumla watamlilia

kila moja angependa kuendelea kuona mchango wake katika bunge lijalo lakin yote ni mapenzi ya Mungu

Mungu awalaze mahali pema marehemu wote na pia awajaze nguvu wanafamilia,jamaa na marafiki wote wawe na uhimili wa msiba huu mkubwa.
 
yaani hii nchi...huku mwamunyange haonekani...huku helkopta ya filikunjombe...huku kigoda kafariki,kuke mtikila,Kule kombani...Mara emmanuel makaidi
 
Januu Wari ashitakiwe kwa makosa ya kimtandao kutoa taarifa potofu!Hata penye ukweli bado wanaleta mahaba nyambaf zake.

Kwa tz ngumu na ukitegemea yupo kundi la wezi wenzie wasiojali. ..msiba huu ni mkubwa kwetu Kwa maana jamaa alikuwa jembe Kwa ss wananchi. .kafanya mengi mno mazur. .watu kama January hawana faida zaid ya kuropoka ovyo
 
Pumzika kwa amani uliyekuwa Waziri Mkuu wangu mtarajiwa Hon Deo
 
Deo Filikunjombe kalale mahala pema. Uliwatendea wananchi wako haki kweli kweli nina hakika umewaacha kama yatima: Ulikula naoa, ulichimba nao mashimo ya kuweka nguzo za umeme, ulipakua nao cement na mabati toka kwenye malori, nk.

Hakika Ludewa watakuenzi na bila shaka walitamani upate miaka mingine mitano na zaidi ili uwatumikie.
 
Ni kiongozi tulimuitaji katika kipindi hiki si kwa upande wa jimbo lake bali taifa kwa ujumla, alikuwa kiongozi hasiyejiona, aliyeishi maisha ya kitanzania, mchapa kazi, mwadirifu,mtu aliyeamini maendeleo ya jimbo lake ni watu kufanya kazi,aliwapenda watu wote bila kujali,vyama vyao vya siasa,alikuwa tayari kufanya kazi usiku mchana jua na mvua kuwaletea maendeleo wananchi wa tanzania,alichukia wizi na ufisadi na hakupenda makudi,

mungu haujatutendea haki kabisa katika kipindi ambacho taifa letu linaitaji viongozi wa namna hii kwa faida ya watanzania wote,
mungu akupumzishe mahali pema peponi

amina,
 
Huu uzi ngoja nipite kimyakimya, nijifanye kama sijauona vile!!
 
Inasikitisha, haizoeleki, sote tu katika safari hiyo.
Muhimu tuwaombee wapate pumziko. Lakini muhimu zaidi uchunguzi wa kina ufanyike tuweze kujua sababu zilizopelekea ajali hiyo.


Maeneo kadhaa yanaweza kuangaliwa.
Rubani, kuona kamataratibu za kiusalama zilifuatwa kabla ya kurusha chombo; taratibu zinatuambia iwapo rubani ataona au kuhisi kuna chochote kinachotia shaka, anapaswa kusitisha safari kwa muda kupisha wakaguzi wachunguze na wajiridhishe.
Wakufunzi, watusaidie kuona kama hawa marubani wetu wanapata marudio/muhtasari wa tahadhari za kazi yao kila wakati kama sheria zinavoelekeza.
Waongoza Ndege, wanawezak usaidia kuonyesha hali aliyokuwa nayo Rubani kabla ya kurusha chombo, katika maongezi yao ya mwisho na kama kuna chochote walimshauri.
Mafuta, ufanyike uchunguzi wa mafuta yaliotumiwa na chombo (yaliobaki/yaliyo kwenye kihidhadhio) kuona kama hayakuwa yameathirika kwa namna yoyote ile.
Wakaguzi wa chombo, wahojiwe kuona kama walikagua chombo ipasavyo kabla ya kukiruhusu kiondoke.

Records za chombo husika.
 
R.I.P Deo na slaa.Tuombe sana jamani huu mwaka viongozi wengi wametangulia mbele ya haki.
 
Deo kati ya wapiga picha bora enzi zile Makelele University ukaja kua kiongozi bora kwenye jimbo lako duh siku zinakimbia sana ni kama jana ila wewe haupo tena.
Pumzika kwa amani comrade naamini umeacha alama chanya kwenye jamii yetu.
 
Mkuu,

that was my first reaction... lakini kama tunaamini, tujue kwamba Mungu huona tusiyoona

It is a sad loss... RIP Deo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…