Elections 2010 Helkopta ya JK yakwama kutua Ngara, ahairisha mkutano


Hizo data si issue, tunaweza hata kuwauliza watu walio on the ground wakatuambia. Huwezi kuwa na hali ambayo hairuhusu helikopta kutua halafu ukawa na watu kibao wako mkutanoni wanamsubiri rais, haiingii akilini.

Unasema "it could be weather haikuwa nzuri" sawa, lakini utanote unatumia neno "could", sisi tunataka watuambie wanaposema hali ya hewa mbaya wanamaanisha ya wapi ili tuondoe hiyo "could" tupate vitu vya uhakika. Kwa nini tutumie could kwa vitu tunavyoweza ku verify ?

Helikopta haihusiani chochote na uwanja wa ndege, helikopta inaweza kutua hata kwenye uwanja wa mpira au juu ya jengo imara, kwa hiyo habari za uwanja wa ndege hazina uzito hapa. Na hata kama unaongelea habari za hali ya hewa, hata kama ni kweli kwamba nyanja hizi za ndege zinaongoza kwa hali mbaya ya hewa, kitu ambacho hujatuletea source, hii haimaanishi kwamba siku hiyo kulikuwa na hali mbaya ya hewa. Rekodi tofauti hazionyeshi hivyo.
 
Kuna kitu kinafichwa hapa.

Inawezekana helikopta mbovu au Kikwete hali yake bado si nzuri.
 
Mtazamaji

Unataka verifications gani za wanasiasa au za kitaalamu, kama ni za wanasiasa wao wamesema helikopta haikutua kutokana na hali ya hewa, kitaalamu tunatumia vipimo vya aina mbalimbali, mfano Wind speed, humidity, temperature, visibility, na machine technical problem pamoja na uwezo wa pilot wake.

Kulingana na weather forecast ya Ngara /Kagera Av. wind speed 7mph, humidity Av. 30% , visibility av. 30km, temperature av.20degrees C. Hata kama kutakuwa na changes ni kidogo, kwa hali ya hewa kama hii hatutegemei helikopta ishindwe kutua, labda kesho tuambiwe ilitokea catastropihic weather condition ghafla na kuezua nyumba kadhaa.

Mimi ningekubaliana nao labda kama wangesema ilishindwa kutua kwa technical problems za helikopta yenyewe hapo ndipo tungehitaji verifications toka kwa pilot.
 
Huu mwaka unaonekana si mzuri sana kwa JK kwakweli. Jumamosi kaanguka, jana msafara wake umegonga mtoto wa watu (ni vile tu watu wenye hasira kali hawakuwa karibu wamshambulie) tena leo helikopta imegoma kutua. Mwisho wa yote helikopta ita.... tusije tukampote Rais wetu bure. Bora aachie tu ngazi ili aendelee kula mafao yake ya Urais wa miaka mitano.
 
Kweli JK na serikali yake anakazi wa-TZ hawadanganyiki tena....watu wana-data big - up sana
 
Helikopta ya CCM inahitaji runway?

Ingekuwa hali ya hewa inazuia helikopta kutua, basi helikopta zisingetumika kwenye shughuli za uokozi katika hali mbaya ya hewa!
 
Hapa kuna mawili nina ruleout hali ya hewa ambayo haifichiki iko wazi hata pilot huwa anatumia data hizi hizi tulizonazo. Inawezekana helikopta ilikuwa na hitilafu fulani ikalazimika itue ghafla kwa usalama wao au ndani ya helikopta mmoja kati ya hawa wawili aliugua pilot au rais na si abiria mwingine yeyote kusababisha safari ivunjike.
 
Helikopta imeshindwa kutua ina maana rubani kashindwa kutua. Sababu inaweza kuwa Technical or weather may be na Experince ya rubani
Kama ni kweli Helikopta iriruka Kutoka kituo A na kuelekea ngara(kituo B) inawezekana ilishindwa kutua sasa je ilirudi wapi?Je kama helikopta imeshindwa kutua katika mazingira haya what can we conclude?

Inawezekana pia ni makeke ya mwandishi Lada hata Helikopta haikutoka Kituo A kwenda kituo B(Ngara) of wich heading na habari ilitakiwa iwe wazi na sio kutumia neno yashindwa kutua. labda wangesema yashindwa kwenda au yashindwa kundoka.

labda wanajua ni aina na model gani ya helikopta wanatumia watuambie tu google tujue iko equiped na vifaa gani na uwezo wake.
 

Aiseee mhhhhhhhhhhhhhh alisemaje tena mbayumbayu na yule ndege mwingine!!!! aisee 5% humidity, visibility ! Peupeeeeeeeeeeeeee
 
Jamani JeyKey afya yake inazidi kuzorota, amekonda huyo!..Tumuombee huyo aliyekuwa raisi wetu wa awamu ya nne!!..
 

Sasa natambua kwa nini CCM ilikuwa haitaki wananchi wake wapate elimu ya kujikomboa.
 
Sasa natambua kwa nini CCM ilikuwa haitaki wananchi wake wapate elimu ya kujikomboa.

ahaaaa

hapo ndio umegonga ikulu... adui wa watanzania ni ujinga, maradhi na umaskini... lakini rafiki wa ccm na kj ni ujinga, maradhi na umasikini

thats where we get desperate and ill-informed
 
Kuna kitu kinafichwa hapa.

Inawezekana helikopta mbovu au Kikwete hali yake bado si nzuri.
Kuhusu hi helicopter Wote tunasema inawezekana ili au lile lakini kitu ambacho wengi tuko certain nacho ni kuwa Rais wetu JK ni mgonjwa
Hili ya JK kuwa mgonjwa sio inawezekana hilo tuna uhakika nalo.
 
Kuhusu hi helicopter Wote tunasema inawezekana ili au lile lakini kitu ambacho wengi tuko certain nacho ni kuwa Rais wetu JK ni mgonjwa
Hili ya JK kuwa mgonjwa sio inawezekana hilo tuna uhakika nalo.

Kilichowekewa inawezekana si ugonjwa wa JK, bali hali yake ya sasa. Anaweza kuwa mgonjwa lakini anadunda kwa sababu hali yake si mbaya.
 
tatizo nchi hii sisi wenyewe hatujui kiswahili halafu tunajifanya wajuaji......si tafakali,ni tafakari na sio hatu,ni hatua.rudi school :confused2:
 
tatizo nchi hii sisi wenyewe hatujui kiswahili halafu tunajifanya wajuaji......si tafakali,ni tafakari na sio hatu,ni hatua.rudi school :confused2:

Ng'wana Shija ulimhola?

Nimecheka kwa kufurahi maana jirani yangu wa zamani alikwa anaitwa Malembeka na ni Msukuma
 
sasa jamani kama mganga wa serikali kasema JK asipande 'chombo kinachoruka angani' mnategemea mpewe sababu zilizo verifiable?
 
Wanamtafutia sababu mgonjwa wa taifa achoke na kuanguka! asante kutupa taarifa
Hata kama ukimuwazia mabaya haumuwezi. ushindwe kabisa kama unaona dili ugonjwa huo uwe juu jako. wewe ni mgonjwa wa kitongoji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…