Elections 2010 Helkopta ya JK yakwama kutua Ngara, ahairisha mkutano


Angalia picha hiyo wakati natafuta Model yake
 
Hizo ni chuki binafsi na wote wenye hurka kama yako ni wapuuzi,kwa hiyo wewe ni mpuuzi.mchawi, Lakini humlogi mtu na yote ya kipuuzi uliyoyanuwia kwa kiongozi wetu, yawe yako.Chuki yako ikutafune mwenyewe.Wewe si mwana JF mstaarabu hufai, hooovyo.
 
Jamani mbona thread inatoa taarifa tu kuwa helikopta imeshindwa kutua kwa sababu ya hali ya hewa na wengine wanaanza "kupersonalize"? Nadhani mwenye kutujuza alitaka tupate habari kuwa mkutano wa JK wa kampeni ni leo na siyo jana. Na kwa wale wenye kutumia helikopta pia wajihadhairi wakitembelea Ngara.
Mambo ya kuombeana mabaya hayana maana na inaonyesha akili ya mchangia mada isivyopevuka. Kuwa katika kambi tofauti au vyama mbadala siyo chuki bali ni kushindana kwa hoja. Hebu tuondoe mawazo ya upinzani kichwani tubakize ya ushindani. Tuna vyama vya ushindani na si vya upinzani. Na ndiyo maana si kila kitu ambacho CCM inafanya ni kibaya la hasha bali CHADEMA au CUF ingeyafanya labda kwa ufanisi zaidi au kwa njia mbadala na si kwamba wataacha kuyafanya yale yenye tija kwa nchi na watu wake.
Watu wanaogopa kuchagua vyama vya upinzani kwa sababu ya mawazo hasi ya neno "upinzani".
 
Hata mimi nashangaa kwani si tu upinzani bali chuki binafsi.
 

Kituo A helkopita iliporuka ilikjuwa ni Karagwe na baada ya kushindwa kutua Kituo B (Ngara) ilirudi Kituo A (Karagwe) na kusafiri kwa magari. Aliingia jana usiku kwa Magari
 
tatizo nchi hii sisi wenyewe hatujui kiswahili halafu tunajifanya wajuaji......si tafakali,ni tafakari na sio hatu,ni hatua.rudi school :confused2:

Nimepokea mkuu, Tatizo mie Mkurwa na Kiswahili wapi na wapi (R na L) taabu
 
Jamaa alizimika tena, masikini sifa zitamponza angeamua kujitoa tuu,mpaka amalize kampeni domo si litakuwa limemwagika, maana kila akianguka lazima aume mdomo, si mnaona ile ya jumamosi aliposema aiseee kisha akauma mdomo then akadondoka
 
Leonard Mubali, Ngara

KATIKA hali isiyo ya kawaida mgombea urais kupitia CCM,Jakaya Kikwete, jana jioni alishindwa kuwahutubia wakazi wa Wilaya ya Ngara na vitongoji vyake kama ratiba yake ilivyoonyesha baada ya helikopta anayotumia kushindwa kutua eneo hilo.

Katika viwanja vya Posta ya zamani mjini Ngara umati wa watu uliofurika, ulielezwa kuwa Rais Kikwete hataweza kuhutubia hadhara hiyo, kufuatia helikopta iliyopaswa kumchukua wilayani Karagwe kushindwa kutua kwa sababu ya hali mbaya ya hewa.


Akiahirisha kikao hicho cha kampeni majira ya saa 11:30 jioni, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ngara, Hellena Adrian alisema kutokana na hali hiyo, Rais Kikwete alilazimika kutumia njia ya barabara kutoka Karagwe kuelekea Ngara.

Aidha, Adrian aliongeza kuwa Rais Kikwete atahutubia wakazi wa Ngara leo asubuhi, majira ya saa mbili asubuhi kabla ya kuelekea mjini Lulenge kwa ajili ya mkutano wa pili.

Baadhi ya watu waliohojiwa na mwandishi wa habari hizi hususani wale waliokuwa wakimsubiri kumsikiliza mgombea huyo walionesha wasiwasi wao kutokana na kuahirishwa kwa ziara hiyo na kuzua maswali mengi huku wengine wakihusisha na mawazo mengine kabisa.

Source: Mwananchi
 

Waliofia kuanguka tena make hakukuwepo amburance na wabebaji wangekuwa wachache
 
Afya ya kikwete siyo mbovu kama unavyofikiria.madaktari wa ndani na nje ya nchi wameprove kuwa afya yake ni nzuri na vipimo vinaonyesha hivyo.wewe unayesema afya yake ni mbovu umetumia vipimo gani kujua afya ya kikwete? nipe scintific investigation uliyofanya na ukajua kuwa afya yake ni mbovu.acha chuki binafsi zisizokuwa na msingi
 
Hizo ni chuki binafsi na wote wenye hurka kama yako ni wapuuzi,kwa hiyo wewe ni mpuuzi.mchawi, Lakini humlogi mtu na yote ya kipuuzi uliyoyanuwia kwa kiongozi wetu, yawe yako.Chuki yako ikutafune mwenyewe.Wewe si mwana JF mstaarabu hufai, hooovyo.
Nyie mnaotetea ugonjwa wa rais ndio mnaomuumiza kwa kumpa vijisifa vya kinafiki eti ana nguvu kweli kadondoka akainuka na kuendelea na mkutano huo ni unafiki. Leo sisi tunaomwambia ukweli apumzike mnatuona hatumpendi siku rais akidondoka na kuzimia kwa muda mrefu sana ndipo mtatuelewa tulikuwa na maana gani.
 

Ona huyu naye! Kazi ipo ukiwa na watanzania kama huyu asiyependa ukweli
 
Nimempigia cm mshikaji wangu aliyeko Ngara. anasema kwa sasa ni kiangazi, huu ni wakati wa kuanika kahawa na mavuno mengine. kipindi hiki hutumika kwa ajili ya sherehe na tafrija mbalimbali kwa kuwa ndo kuna hali nzuri kuliko vipindi vingine.

Sasa hiyo hali ya hewa ilitakiwa ipi tena? Mambo yalimshika tena huko angani. Make ingetua na watu wasione mkulu anachomoka kwenye hiyo kitu ingeleta skendo tena. Japo bado imezua utata
 

Inawezekana ndo unaamka! Unataka tulembe nini wakati una mgonjwa? Wazima hamkuwaona kama mnataka walio safi?
 
Eti afya yake ni nzuri unafiki mtupu, mtu unatoka hospitalini unapepesuka na kuanguka mlangoni bado unasema una afya nzuri. Mtu kaanguka tena mbele ya kadamnasi wote tumeona, angejikwaa tungejuwa kajikwaa lakini kaanguka kwa kuishiwa kinga za nguvu mwilini sio ukimwi bado unataka scientific investigation. Sielewi una maana gani unaposema hivyo au una maana ya postmortem.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…