kwa wanaofahamu naomba msaada, nimekuwa mkandarasi mdogo mdogo kwa muda, bila ya kuwa na kampuni napiga vikazi vya ujenzi wa mashule vijijini, sasa nimeona nimekuwa kimtaji, nahitaji kuwa na kampuni na leseni ili niweze kupata kazi kubwa, sasa kupata leseni ndo sijui nianzie wp? wanajf naamini mtanipa muongozo mzuri.
mkuu kwanza hongera kwa kuamua kuacha kuibia serikali ya mafisadi kupata usajili ni rahisi tu sajili kampuni kwanza brela kisha nenda tra kupata tin no kisha unakwenda jiji kufatilia leseni maelezo mazuri utakuwa unayapata sehemu husika mkuu

Chain hii inakuhusu kwa 100%. Utaifuata kama ilivyo.
Nenda kasajili Brela
Nenda CRB-Contractors Registration Board
Utaenda TRA
Utamalizia na Leseni.
Ndugu yangu kwote utapita kama unakula ugali wa mhogo na mlenda. Kazi kubwa ipo CRB. inatakiwa ujipange. Kanunue form ndipo utajua unatakiwa ufanye nini. Ila unaweza tembelea Mtandao wao.