Si mara zote ni lazima kuanzisha kampuni. Kama lengo ni kufanya biashara una weza pia kufanya kama mtu binafsi (sole propriatorship) au kwa kushirikiana na wengine (Partnership). ubaya wa kampuni, inakuwa na compliance requirements nyingi amabazo in some cases zinaweza kukudistract.
Kwa kusaidia kujibu swali lako. Cha kwanza ni kuisajiri (incorporation) hiyo kampuni BRELA (
www.brela-tz.org). Katika hiyo process utatakiwa kuandaa Memorandum of Association (katiba inayoelezea umiliki na wamiliki wa kampuni, madhumuni ya kampuni na ukomo wa wajibu) na kama ukitaka Articles of Association (taratibu za kuendesha kampuni).
Baada ya hapo utatakiwa kuisajili kampuni kama kama mlipa kodi (TRA watakupa TIN). Na pia utatakiwa kuomba leseni (inaweza kuwa zaidi ya moja) kuendana na aina ya biashara kampuni itataka kufanya.