Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Hemed Suleiman Abdulla, akihutubia mkutano wa kampeni Septemba 24, 2025 katika eneo la Makombeni, Mkoani, amesema tofauti ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na vyama vingine ni kwamba vyama hivyo havina cha kueleza walichokifanya kwa wananchi, na bahati mbaya havielezi pia nini vitakavyofanya.
Aliongeza kuwa, “Wanahubiri chuki, wanahubiri fujo, wanahubiri uvunjifu wa amani.”