Hemedy PhD adai watoto wake 6 wamepishana miezi miwili, miwili tu

Rosh Hashannah

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2017
Posts
3,415
Reaction score
2,043
Msanii wa muziki wa Bongo Flava, Hemedy PhD amefunguka mambo kadhaa kuhusu yeye kuwa baba wa watoto sita.


Muimbaji huyo ambaye anatamba na ngoma ‘January to December’ ameiambia Planet Bongo ya EA Radio katika watoto wake sita alionao wamepishana kila mmoja miezi miwili katika kuzaliwa.

“Mtoto wangu mkubwa ana miaka mitatu waliofuatia wote wanapishana miezi miwili miwili, sitaki drama kila mtu na mama yake lakini all in all nawapenda sana watoto wangu na itakuja siku nitaweka mambo yote wazi kama mnyama future” amesema.

Katika hatua nyingine Hemedy amesema wiki mbili zilizopita girlfriend wake alipata shida na alikuwa amebeba mapacha, hivyo sasa angekuwa na watoto nane akiwa na umri wa miaka 29.
 
Mtoto wa kwanza mpaka wa sita hakuna hata mtu wa kumkanya ktk familia yake?amelelewa ktk familia gani huyu kijana{sisemi mimi ni msafi}ila ni aibu baba au mama kuitwa bibi au babu na watoto waliopatikana kwa njia ya uzinzi,tena wajukuu sita...asijifananishe na sijui Future huyu naamini amelelewa ktk maadili ya kidini huyo role model wake anaweza kuwa haamini uwepo wa Mungu na dhambi ila huyu dogo anao wazazi wanaoamini hivyo na anawatia aibu!sasaivi kijana kumtia demu mimba imekuwa sio hatari tena kwa wazazi bali ushujaa wa-Africa sivyo tulivyo sisi wazazi wawasimamie vijana wao wawape wake wakiona umri umefika!
 
aliongeza rungu baada ya kudharauliwa..sasa anafanya msonesho
 
Kweli ametii agizo la mkulu la kufyatua
 
Yaani kwa miezi miwili wataanza shule mwaka mmoja woote sasa mziki ndo utakuwa hapo, sijui hakuliwaza hilo?
Atawasomesha kijanja janja .hamuwajui Watoto wa mjini hao.apo ata gharamia uniform tu.mtoto anasoma Shule nzuri kbsa
 
Sasa na yeye anaona sifa!Mungu tusaidie ndio vijana wetu hao.Wewe watoto sita inamaana ukitumia Kinga ,pili watoto sita kwa usawa upi utawalea au Ni starehe tu.Ukimwi has long way to go jamani Kama hizi ndio tabia zetu
 
Nipo Mlimani City nimemkuta mdada anajimiminia bia moja baada ya nyingine kwa hasira. Namuuliza kulikoni ndugu yangu, mbona bado asubuhi na mapema hivi? Ananiambia, "We fikiria uncle, nna maboy friend wangu hawa, watatu. Huyu mmoja nilimpenda sana nilikuwa nafikiria one day tutaoana. Yaani ndio nimekuja kugundua kumbe ananicheat na wanawake wengine. Uncle hapo ungekuwa wewe ungejisikiaje? ".
Inabidi na mimi niagize mzinga wa konyagi ili niendelee kutafakari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…