Henry Ford heshima zikufikie popote ulipo

Henry Ford heshima zikufikie popote ulipo

denniehanda

Member
Joined
Apr 11, 2019
Posts
12
Reaction score
28
Nipo Google natafuta lilipo sanamu la Henry Ford, napewa majibu kuwa lipo mji mdogo wa greenfield, Michigan mahali yalipo Makumbusho yake. Bado najichanga nifike ilipo lala akili kubwa ya magari.

Nikajiuliza watu wana historia gani kuhusu Henry Ford, huwenda hakawa darasa bora kwa watu wa magari wa kizazi hiki?

Ni miaka mingi imepita tangu afariki, amefikisha miaka 73 ndani ya kaburi. Imeandikwa kazaliwa mwaka 1863 akafariki 1947 'Lo Siento Henry'[emoji17]. Tasnia ya Magari ishaanza kumsahau Henry, itakumbukwa alikua mtu wa kwanza kuzalisha magari kwa ajili ya biashara 'mass production', alisaidiwa na Assembly Line aliyogundua yeye. He was the Real Deal

Mpaka kufikia Mwaka 1924 alikuwa ameshazalisha magari aina ya Ford Model T zaidi ya milioni 10. Mfumo wake uliwafanya mpaka watu wa uwezo wa chini waweze kumiliki gari. Historia iliandikwa mpaka kwenye kitabu cha Rekodi za dunia Cha Guiness.

Ford ni mfano wa kuigwa kila eneo, alikuwa Baba Bora, Msomi, mfanyabiashara, mwanafalsafa, mtu wa siasa pia Alikosoa sana vita ya kwanza ya Dunia.

Kila kijiji kina wazee bwana, Kwenye kijiji chetu cha magari Ford anasimama kama mzee mwenye Busara Sana. Aliisaidia Marekani na Dunia nzima Kwenye usafirishaji, biashara na hata mahusiano ya kimataifa kupitia Biashara ya Magari Ulimwengu mzima.

Rafiki zangu wajerumani bado wabishi sana, bado wana imani kila linapotajwa neno gari, wanatajwa wao. Watuache kidogo tunamalizia nyimbo ya shujaa wetu Henry. [emoji445][emoji445]Glory Glory Henry [emoji445]

#KibiMakala

Tufollow Instagram [emoji116][emoji116][emoji116]



kibitechnologies-20200402-0002.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
RESPECT KWAKE AMETULETEA BIDHAA AMBAYO INAWAFANYA WALE VIUMBE WAPAGAWE UKIWA NAYO
 
hapa bongo tuna nyumbu ila mtengenezaji wa hizi gari simjui
 
Back
Top Bottom