Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,621
- 8,411

Kuelekea kuanza kwa msimu mpya wa ligi, wachambuzi wa soka katika kituo cha runinga cha Sky Sports wametoa utabiri wao timu itakayotwaa ubingwa na zile zitakazomaliza katika nafasi nne za juu.
Katika utabiri wao, wachambuzi hao ambao ni Thierry Henry, Gary Neville na Jamie Carragher wameiondoa kabisa Leicester katika kinyang’anyiro hicho.
Badala yake, wametupia karata yao ya ubingwa kwa vilabu vya jiji la Manchester. Kitu ambacho kimsingi si cha kushangaza, ukizingatia namna walivyofanya usajili wao kuanzia makocha mpaka wachezaji.
THIERRY HENRY
- Man City 2. Man Utd. 3. Chelsea 4. Arsenal
“Chelsea hawatakuwa na Michuano yoyote ya Ulaya, hivyo itakuwa faida kwao, lakini inaweza kuchukua muda kidogo kuendana na kile anachowafundisha Conte.
“Vivyo hivyo kwa Mourinho na Man Utd. Vilevile City na Guardiola- hivyo basi, labda kuna upenyo kwa Liverpool, Arsenal na Tottenham – ambao wamekuwa na vikosi vyao vile vile pamoja na makocha wale wale.”
GARY NEVILLE
- Man Utd 2. Arsenal 3. Man City 4. Liverpool
“Kuna wachezaji ambao wanavaa tisheti za United na kuwaingia kwenye mioyo yao na kupambana kwa nguvu – na hiyo sasa ndiyo Manchester United inavyopaswa kuwa.
“Kwangu mimi, bingwa atakuwa Man Utd, Arsenal nafasi ya pili Arsenal, Manchester City nafasi ya tatu na Liverpool nafasi ya nne.
JAMIE CARRAGHER
- Man City 2. Chelsea 3. Man Utd 4. Liverpool
“Bila shaka, wanahitaji kusajili zaidi, lakini tayari wana wachezaji ambao wako vizuri tangu hapo awali kama David Silva, Sergio Aguero na Kevin De Bruyne. Hawa watatu watakuwa ni mwanga kwa wengine watakaokuja.
“Kwa kuwa hawashiriki kwenye michuano yoyote ya Ulaya, nadhani Chelsea watafanya vizuri kwasababu watakuwa na muda mwingi wa kuzoeana mazoezini. Na tukumbuke kwamba ni miezi 12 tu imepita tangu wawe mabingwa, vilvile Antonio Conte ni kocha wa kiwango cha juu.
“Nadhani Liverpool pia watanufaika kutokana na kutokuwa na Mashindano ya Ulaya.”