Heri aibu kuliko kifo (Kisa cha robbot)

STUNTER

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2015
Posts
13,076
Reaction score
17,247
Mke kasikia mumewe ambaye alikuwa safari
akigonga mlango wa nyumba yao afunguliwe,
naye alikuwa na bwana mbaya zaidi walikuwa
wanaishi ghorofa ya kumi na nne, mdada
mwasherati akamwambia bwana waliekuwa nae, aisee mume wangu karudi, hebu simama jifanye robot,
niachie mie nizungumze; usitikise,

MKE: Karibu mume wangu. Mume akaingia
akakuta mtu yuko uchi kasimama;

MUME: Huyu nani?

MKE: Hilo robot nilinunua linanisaidia kujiliwaza wakati wewe haupo.

MUME: Okay poa, sasa mwenyewe nimerudi na
mimi nahamu sana na wewe, nipe halali yangu

MKE: Samahani mume wangu, niko siku mbaya
pole kwa leo. Ngoja nikutengenezee chai...wakati
mke yuko jikoni anatengeneza chai;
MUME: (Akawa anaongea peke yake) Dah mke wangu
hawezi na mimi nataka, ngoja
nilishughulikie hili robot la mke wangu...... jamaa
mgoni kusikia vile akajua hatari inakuja, akaanza
kuongea kwa sauti ya kirobot;

ROBOT: Robot bovu halifai, robot bovu halifai
MUME: Duh mi ninahamu hata robot nalo bovu,
upumbafu sasa silinajaza tu nafasi humu? kama
bovu ngoja nilitupe nje....Jamaa Robot akajua kifo
kinakuja, gorofa ya kumi na nne mchezo? akaona
ajisevu; heri aibu kuliko kifo

ROBOT: Robot limepona, robot limepona halina matatizo, halina matatizo
 
Kwa hiyo jamaa alifanywaje mkuu? Kweli mke wa mtu sumu japo mtamu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…