Heri ya mwaka mpya , Heri ya Kumbukizi ya Kuzaliwa kwangu!

Chibule

Senior Member
Joined
Sep 25, 2024
Posts
171
Reaction score
230
Ikiwa Leo ni Kumbukizi ya Kuzaliwa kwangu, Umri ukiwa umesogea sana nimeona niwaachie ujumbe kidogo

Maisha yanapokupa baraka nyingi usikimbilie kusema wenzako ni Wavivu, watu wapo kimya hawasemi tu ila wanapigana vita nyingi sana na wanafeli ila hawalalamiki, ukipata shukuru.

Mwanangu wewe ni Mwanaume, usimpigie simu zaidi ya mara mbili, usimwombe sana mpaka akachoka, fanya kitu kwa kiasi linda mipaka yako kwa hoja ya Uanaume, unyonge huleta dharau.

Mkubwa uliyopo kwenye ajira, jifanyie utamaduni mzuri wa maisha! Usiende kazini kusengenya, usiseme watu vibaya, wewe fanya kazi yako kwa bidii, subiri mshahara wako urudi nyumbani ukafurahi na familia yako.

Kwenye maisha usisahau kuishi, wastani wa kuishi kwa Mtanzania ni miaka 60! Utagundua mpaka unahitimu Chuo Kikuu ushapiga nusu ya maisha, tuna muda mchache wa kuishi! Tusisahau KUISHI, chuki ni mzigo achana nazo, kwenye baya na zuri tabasamu na sema Amina .

Mpambanaji, Mama yupo nyumbani anapiga goti kwa Mungu kulilia mafanikio yako, ila wewe unamsaliti sana ni jana tu unapiga goti kumlilia Mwanamke! Hakuna aliyekuibia Manzi yako, sema yeye alimchagua Jamaa dhidi yako, hilo limeisha jiwazie mwenyewe sasa.

Wanangu usimkatishe tamaa Bonge aliyeanza Gym kukata mafuta, usimcheke Chembamba anayebeba chuma kujenga mwili na wala usimsanifu Mchizi anayeanza biashara yake mdogo mdogo, unahitaji uthubutu kwenye kuanza chochote, tukionana kwenye mapambano tupeane tano, maisha ndio yalivyo Kila mtu na Bahati Yake

Heri ya mwaka mpya 2025.
 
Kwako pia kaka ,ahsante kwa maneno kuntu
 
Back
Top Bottom