Heri yake Mwalimu!

Heri yake Mwalimu!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
33,771
Reaction score
41,027
Hiki chama cha Mwalimu
Hakina tena nidhamu
Tunu iliyo adimu
Nani wa kumlaumu?

Anayo heri Mwalimu
Kwani sasa marehemu
Kutoona udhalimu
Hakika leo kigumu.

Kimepoteza hatamu
Na sasa hakina hamu
Watukanana kwa zamu
Kwenye Chama cha Mwalimu

Wasomi na wataalamu
Wafuasi wake Mwalimu
Wajanja na chakaramu
Chaweza vipi kudumu?

Walipuana mabomu
Ya siri twayafahamu
Dalili za uazimu
Maskini Sisiemu.

Yu wapi mtu timamu
Hayupo Dar-es-Salamu
Ndani yake Sisiemu
Mpaka twende huko Lamu?

Wenzangu na mfahamu.
Tumeandika kolamu,
Na tumetuma salamu
Kumbe sisiemu ngumu

Vipi tutawaheshimu
Sisi wana wa Adamu
Mafisadi wadhalimu
Kwenye chama cha Mwalimu

Siyo tena cha muhimu
Kukipa tena hatamu
Tusiwe hivyo karimu
Jukumu hili adhimu

Na tupandishe alamu
Ya ujumbe maalumu
Wasikie sisiemu
Hatujageuka Utamu!

Tuache kutabasamu
Tukikenua kwa zamu
Aibu ya Sisiemu
Tanzania yetu humu.

Twapaliza baragumu
Twakemea Sisiemu
Mmemwaga yenu sumu
Nchi imekuwa ngumu!

Isije kuwa lazimu
Watu wakamwaga damu
Kisa hii sisiemu
Ivyopoteza hatamu!

Tutabaki kushutumu
Nani wa kumlaumu
Na jumbe za kwenye simu
Hadi ngoma za msimu!

Kikwete mambo magumu
Kaishindwa Sisiemu
Nani atamlaumu
Vigogo wakishutumu?

Tumejawa na magamu
Sababu ya sisiemu
Hiki chama cha mwalimu
Tukubali kusalimu?

Moyo umeshikwa ghamu
Chakula sinacho hamu
Hakuna kilo kitamu
Natamani ninywe sumu!

Nchi itatugharimu
Kosa lao Sisiemu
Kwenda mbele ni kugumu
Tukiwaachia humu!

Haliendi gurudumu
Kisa hawa sisiemu
Tumefikia patamu
Sasa tutawahukumu.

Naweka chini kalamu
Nijiunge sisiemu?
Kwenye chama cha Mwalimu
Kuing'oa hii sumu?

Ama mtanilaumu?

Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)
 
Big-Up Mkjj for a very interesting poem!

Babu zetu walinambia Sikio la kufa halisikii dawa!

Yaliyoongelewa vyumbani sasa yanapatikana masokoni na kwenye Njiapanda za miji!

Hivi hawa ndugu zetu, pamoja na kuadhiriana huko walikofanya, bado watashikamana tena kama chama na kushinda uchaguzi 2010?

Watatushinda tukiwa bado hai au maiti zinazotembea?

Mungu bariki Tanzania, tuongoze vyema katika uchaguzi huo!
 
Mkjj, hongera kaka shairi zuri japo sijidanganyi kuwa wakati unaliandika ulikuwa na tabasamu usoni. najua uchungu wa kusalitiwa na hawa wahuni, forgive my language. aluta continua, if we must day, lets not die like hogs...
 
Nani wa kuku Laumu?
Kila mtu baragumu
Nchi imekuwa Ngumu
Sasa twende Lamu
 
[ame]http://www.youtube.com/watch?v=8MYhp-2-Flc&feature=related[/ame]
 
Kila siku twalaumu
Viongozi wamekosa nidhamu,
Ufisadi washika hatamu,
mpaka kukosa adabu.
 
Naweka chini kalamu
Nijiunge sisiemu?
Kwenye chama cha Mwalimu
Kuing’oa hii sumu?

Ama mtanilaumu?

Una beep eeh! watakupigia sasa hivi.....
 
IF u can't fight them join them...inaweza saidia pia to win the bottle.
 
Una beep eeh! watakupigia sasa hivi.....


Kwa nini umem single out Zitto wakati na Mwanakijiji kaandika ? Zitto ni mtanzanoa ana hali ya maoni yake juu ya Kyame Kyenu hiki kya kutuibia na kuonyesha maajabu ya Kilimo Kwanza .Kila mara mnabadili Kauli mbiu wacha tuone baada ya Kilimo kwanza itakuwaje
 
Kwa nini umem single out Zitto wakati na Mwanakijiji kaandika ? Zitto ni mtanzanoa ana hali ya maoni yake juu ya Kyame Kyenu hiki kya kutuibia na kuonyesha maajabu ya Kilimo Kwanza .Kila mara mnabadili Kauli mbiu wacha tuone baada ya Kilimo kwanza itakuwaje


Lunyungu uwe unasoma kwanza na halafu try to engage ur brain before kukurupuka ovyo. Wapi nimem single out Zitto? Hiyo quote yangu hapo juu unajua ni ya nani?
 
Lunyungu uwe unasoma kwanza na halafu try to engage ur brain before kukurupuka ovyo. Wapi nimem single out Zitto? Hiyo quote yangu hapo juu unajua ni ya nani?


Tulieni jamani. Tuzungumze kwa furaha. Lunyungu - Masatu alisema Mwanakijiji anabipu na sio mimi. Masatu anaju mie siwezi kuwabip na lichama lao ambalo ndani yake kuna vyama 7

Lunyungu mtake radhi Masatu maana umemvamia
 
Lunyungu uwe unasoma kwanza na halafu try to engage ur brain before kukurupuka ovyo. Wapi nimem single out Zitto? Hiyo quote yangu hapo juu unajua ni ya nani?


Nakutaka radhi Mkuu Masatu nimesoma vibaya . Tuendelee sasa mbele .
 
Najaribu kutengeneza scenario kichwani ya CCM kumeguka. Nani watakaoondoka? Mafisadi au wapambanaji? Wakiondoka mafisadi hakuna kumeguka. Nani atapoteza muda kuwafuata? lakini wakiondoka wapambanaji then CCM itakuwa vipande. Just thinking aloud!
 
Sisiemu haimeguki kwa kuombewa na kungojewa; sisiemu itavunjika kwa kusukumwa! - quote me!
 
ukijiunga na sisiemu
utakuwa umetuhujumu
uliyohukumu sisiemu
ni sawa na dhalimu

vita hii ni ngumu
kupigana uwe mgumu
kamanda wa foramu
wataka kutujuhumu?

mbali tumetokea
ufisadi kuukemea
leo wachechemea
ufisadi kuuendea?

hakuna kusalimu
sisiemu ni wadhalimu
mapambano humu humu
kumuenzi Mwalimu


............duuh hii kazi ya tenzi ni ngumu sana.......
 
kwa kweli mwenzenu nimeshaomba kadi kabisa... kwa sababu wanaamini tunashindwa kupambana nao humo humo CCM.. nyie ngojeni.
 
Back
Top Bottom