Herufi E inaendelea kufanya vizuri sana sokoni

DATAZ

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2012
Posts
3,799
Reaction score
10,196
Hadi Sasa plate number zinasoma EH... ikiwa ni miezi 6 tu toka herufi E kuzinduliwa.
Inasemekana Kila herufi ndani ya herufi kuu Inabeba magari 1000. Hivyo toka Herufi E Imeanza tumeagiza magari 8000 na zaidi ndani ya miezi 6.

Hongera sana Serikali yetu tukufu kwa kufungua uchumi. Namuomba Mungu herufi ya Jina langu isianze kabla sijavuta mkoko na Mie, INSHALLAH.
 
Tupo M60. Badooo, watengeneze barabara kodi za magari zipungue ndo utaona shughuli. Pesa nyingi sana itatengenezwa kupitia mafuta, gesi, bima na mazao yote ya gari.
 
Namba E imeanza mwaka juzi mwishoni, so ina zaidi ya miezi 6.
 
Wengi wanakopa sana, baada ya hapo wanakuja hapa kulia ugumu wa maisha.

Watu wako 2024 ila washakula hela ya 2030.
 
Juzi nikakutana na land cruiser GXR mpya eti ni namba A ..

1. Hiyo ikiwa ni bus eti, LATRA hawataki kuiona Stendi Mwenge.

2. Washauriwe kutojifungia maofisini, wapate kuyaona mema ya nchi.

3. Nani kasema gari namba? Mbona madude haya:



4. Yamejaa mtaani jezi mgongoni AAA?!
 
Ndo ujifunze sio kukaa kulalamikia mara maisha magumu, mara hamna hela, mara uchumi umeshuka. Pambana, namba E ni uthibitisho tosha hela ipo mitaani ya kutosha tu, ni kujiwajibisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…