Huyu Heri Sasii ametolewa tu kafara! Mbona Japhet Smart naye alivurunda kwenye mechi ya Namungo dhidi ya simba. Kadi yake nyekundu ya utata kwa mchezaji wa Namungo ilifutwa! Ila yeye hakuguswa!Kefa kayombo kaachwa
Hii wametuma ujumbe, kwa tarehe 15 kuwa hawacheki na Mtu lakini hii kaonewa tu.Huyu Heri Sasii ametolewa tu kafara! Mbona Japhet Smart naye alivurunda kwenye mechi ya Namungo dhidi ya simba. Kadi yake nyekundu ya utata kwa mchezaji wa Namungo ilifutwa! Ila yeye hakuguswa!
Kwenye hii mechi aliyofungiwa, na mwamuzi msaidizi wa pembeni anahusika kwenye ile penati ya kwanza. Ila yeye hajaguswa.
Kitu kingine baada ya hili la Waamuzi ni kutungwa Kanuni Wanasiasa wakome kuingilia Mechi za soka mikoani labda wawe viongozi wa timu.Angalau timu underdogs zimeanza kujitambua..
Hii ni matokeo ya reaction ya timu ndogo kutishia kususia ligi..
Vinginevyo wangeacha upepo upite, na baadae maisha yaendelee.
Nilishaandika nyuzi kibao kushauri timu ndogo zitishie kususia kumaliza mechi zilizosalia...ili mamlaka za mpira somo liwaingie....
it was done on deliberate.
Kajiroga au Mchawi ni yeye mwenyewe kuendekeza tamaa badala ya weledi.Akijitambua tu atakuwa Bora kuliko alivyokuwa mwanzo.Ukiiongelea ligi ya Tanzania mwaka 2020-2022 hutaacha kuongelea umahiri wa Waamuzi mahiri na wa kutegemewa kipindi hicho wakiongozwa na Hery Sasii. Sasii alikuwa mwamuzi makini na aliyetegemewa katika Mechi ngumu na zenye ushindani. Kila mpenda soka alifurahia uchezeshaji wake.
Lakini ghafla akaanza kuporomoka na akishindwa kumudu hata Mechi ndogo za Mtibwa Vs Prison.
Jana kafungiwa miezi 6 Kwa makosa ya Wazi aliyoyafanya Mechi ya Simba Vs Singida BS. Ufanisi wa binadamu uko kama wa mashine kuna kipindi unashuka mpaka chini kabisa. Kwa heri Sasii refa wangu bora uliyeanguka ghafla kiufanisi.