Hesabu za matipper ya Mchanga

ben van mike

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2010
Posts
467
Reaction score
190
Wadau naomba msaada wenu kidogo kwenye hii biashara ya malori ya kubeba mchanga na kokoto , hesabu kwa siku kwa lorry la tonne 7, 18 na 32 ni kiasi gani ? Katika hayo yapi yana demand sana ?

Natanguliza shukrani
 
Inategemea na Maeneo ambayo gari itafanyia kazi.

Kwa Dar maeneo ya kazi ni Mbagala, Gongolamboto, kigamboni na Bunju.

Kwa Bunju ton 4 ni 60,000/70,000. Tone 16 ni 120,000/150,000 na Tone 32 ni 250,000 hadi 300,000.

Tone saba kwa huku zimepotea kabisa. Zimebaki Iveco Cargo chache ambazo zinashindwa kuhumili mikikimikiki ya kazi za mjini.

Usisahau kuna watu wa Tanroads wanapima mizani barabarani. Ukikamatwa fine zao minimum 2mil maxmum 6mil.

Ni Pm kwa zaidi.
 

da mbona kiasi ni kidogo sana kiongozi!
 
da mbona kiasi ni kidogo sana kiongozi!

Eeeh kumbuka, wewe ndio tajiri ukiamua gari yako ifanye kazi usiku na mchana utapata double ya hizo pesa.

NB: usiku na mchana ni kwa 32 Tones only.

Kunachoangusha ni wakala wa Barabara (tanroads) kila siku lazima waje na fine zao kama nilivyokueleza. Kwa hiyo michakato mingi inakuwa huku kwa huku tu.

Lakini si mbaya kwa Investment ya 120mil kukupa return ya 7.2mil a month. Kama ukibahatika kupata gari nzuri. In a year unaweza pata 86mil. Na hapo ni tu kama gari unafanya kazi day time. Kama itakuwa inakesha means unapata pesa twice japokuwa gari inachoka haraka.
 

Maneno haya yanavutia laki uhondo wa ngoma uingie ucheze.
 
Ni kweli mkuu investment ni ndefu 120m si mchezo , demand IPO ?
 
Vipi ukiweka tracking system kuna mdau alisema humu laki 3 kwa mwaka au wabongo washagundua jinsi ya kuchakachua
 

je hivi vi canter tani 2 au 3 hesabu yake ikoje???
 
Wakuu hii niliuliza week mbili zilizopita. Mimi nataka kufuata mwenyewe machine nchini UK. Jee mnadhani ushuru wake upoje? nataka tani 32 scania au DAF
 
mkuu labda uingize details kwenye website ya tra , inaonekana Scania ndio nzuri ,
 

Bei ya kokoto ikoje mkuu, kokoto ya Chalinze na kokoto ya Pwani (Kunduchi)
 
je hivi vi canter tani 2 au 3 hesabu yake ikoje???

Swali zuri, hata mi nnayo tani 3 kutoka UK hajafanya kazi hapa nchini.

Nimejaribu kuongea na madereva wa vijiweni Bunju, wengi wao offer yao ni between 40,000 to 50,000 kwa siku.

Kuna jamaa mwingine yeye anafanya shughuli zake Chanika/Masaki kuja Buguruni. Anasema kwa trip ni between 200,000 na 250,000. Niko kwenye dilemma. Sijui niipeleke Chanika au niiache Kijiweni

Pia kuna ishu za minara nazo nasikia nzuri ila wadau wake ni shida kuwapata.

Uchunguzi unaendelea , ntawajuza.
 
Wakuu kama napiga mwenyewe kilungu, maana dereva mwenyewe jee kuununua huu mchanga unaendaje kwa mende moja. Najua bei ya kuuza ni 250,000. Jee machimboni unauzwaje?
 
Wakuu kama napiga mwenyewe kilungu, maana dereva mwenyewe jee kuununua huu mchanga unaendaje kwa mende moja. Najua bei ya kuuza ni 250,000. Jee machimboni unauzwaje?

Kati ya 50,000 na 60,000 na 5000 ya TMAA

Hiyo ni huku kwetu, sijui mahali pengine.
 
gud,nimeielewa hiiii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…