ameline
JF-Expert Member
- Jan 8, 2013
- 2,292
- 1,151
Nashindwa kuelewa serikali ina mpango gani na walimu jamani? mtu anajitahidi kusoma kacertificate kake au kadiploma, au hata kadegree kamoja jamani kwa tabu zake zoote, wengine kwa kuungaunga wengine kwa kuunganisha anabahatika kuchaguliwa then unampeleka sehemu kama hii kweli?? hebu chunguza hilo eneo kama utampata hat mkaza mjomba wa raisi kikwete au hata mawaziri au kiongozi yeyote wa kisiasa, nani atakaekubali ndugu yake alale kwenye nyumba kama hii? Mimi siyo mwalimu lakini ninaumia sana ninapopata taarifa kama hizi, mara ooh mwalimu mkuu kaangukiwa na nyumba, mara oooh mwalimu anaishi ofisini,. this is too much! kama mtu anashindwa kukufanyia dogo kama hili jamani utatarajia kubwa litoke wapi? hebu wananchi tuamke jamani, tunajua kuna mambo meengi sana yamefanywa na serikali ili kuboresha elimu lakini kwa hili, hamjaniambia kitu,. kuna msemo tunaoutumiaga kule uchagani unasema hivii..."UKUNDI MANYA KYA NUMBA AMBIYA KYICHUMI" maana yake ni kwamba ukitaka kujua kilicho nyumbani mwa mtu angalia mlango wa kuingilia, au angalia getini mazingira utakayoyaona ndivyo nyumbani kulivyo,.sasa kweli mwalimu ataishi kwenye nyumba kama hii then elimu ifanikiwe vip hapa? mwanafunzi atashindwa kuingia form one bila kujua kusoma? ari ya kufundisha ipo wapi? tusidanganyane bwana, kama ni kuboresha elimu tusifanye theoritically bali tujaribu kupractice kweli,.Tusiishie kutazama chama tu jamani tuangalie na watu waliomo huko kwenye chama, tuache unafiki, tuungane kuleta mabadiliko.
[h=3]hii ndio nyumba ya mwalimu mkuu iliyobolewa na mvua.[/h]
Nyumba ya mwalimu mkuu Chilaile wilaya ya Nachingwea yabomolewa na mvua
Wanafunzi wakimjengea mwalimu mkuu baada ya kubomolewa na mvua
Hebu niambieni wadau jamani kwa mtindo huu tutafika kweli? madogo wanaacha kusoma wanajenga nyumba, jamaniiii????:A S cry:
[h=3]hii ndio nyumba ya mwalimu mkuu iliyobolewa na mvua.[/h]
Nyumba ya mwalimu mkuu Chilaile wilaya ya Nachingwea yabomolewa na mvua
Wanafunzi wakimjengea mwalimu mkuu baada ya kubomolewa na mvua
Hebu niambieni wadau jamani kwa mtindo huu tutafika kweli? madogo wanaacha kusoma wanajenga nyumba, jamaniiii????:A S cry: