Heshima kwenu Madrid!!

Kiduduye

Member
Joined
Jul 25, 2012
Posts
10
Reaction score
7
Maisha siku zote huwa yanakwenda kwa kasi mnooo, mara baada ya Madrid kuchukua ubingwa 2002 Walistruggle sana kuhakikisha wanarejesha makali yao ambayo tulizoea kuyaona baada ya pale msimu uliofuata 2003 walijitahidi wakachukua La Liga kwenye siku ya mwsho baada ya viongoz wa ligi kwa kipind kirefu Real Sociedad ya Nihat Kahveci kufungwa mechi ya mwisho ya Ligi.

Ajabu ni kwamba baada ya Madrid kuchukua ubingwa wakamuondoa Kocha wao Vicente Del Bosque, Wakamchukua aliyekuwa kocha msaidizi wa Man Utd wakat huo Carlos Quieroz ambaye ni kocha wa sasa wa timu ya Taifa ya Iran, kocha huyu hakuwa na mafanikio ikiwepo kushika nafasi ya nne kwenye Laliga nyuma ya Valencia(Mabingwa) Barcelona na Super Depor ya Javier Irureta, wakajitutumua wakaishia hatua ya robo fainali ambapo wakatolewa na As Monaco.

Quieroz Kaondolewa na nafasi yake kuchukua Jose Antonio Camacho lakini pia naye hakudumu sana nafasi yake akachukua Mariano Garcia Remon. Ilipofika Dec 2005 Wakamtangaza Vanderei Luxemburgo kuwa kocha wao na walifanikiwa kutinga hatua ya 16 bora na kupigwa na Juventus katika hatua hiyo.

2005/2006: Bado pia haukuwa msimu mzuri kwao chini ya mwalimu Juan Ramon Lopez Caro wakaishia hatua ya 16 bora pia walitolewa na Arsenal.

2006/2007: Huu ulikuwa mtawala mpya wa Rais Ramon Calderon, wakamteua Fabio Cappello kuwa kocha ambaye aliwasaidia kuchukua taji la La Liga ambalo walilikosa kwa muda mrefu , lakin kwenye uefa kama kawaida yao waliishia hatua ile ile ya 16 bora baada ya kutolewa na Bayern Munich.

2007/2008: Walifanikiwa kutetea taji lao la La Liga lakin wakaishia 16 bora tena uefa wakitolewa na AS Roma wakiongozwa na Kocha Bernd Schuster.

2008/2009: Walimaliza msimu na mwalimu mpya Juande Ramos ambaye alipigwa 6-2 pale pale Bernabeu na Fc Barca walikosa ubingwa wa La Liga pia Uefa waliishia hatua yao ile ile waliyoizoea ya 16 bora wakitolewa na Liverpool.

2009/2010: Walimuajiri Manuel Pallegrin lkn hawakufanya vizur licha ya kuwasajil Ronaldo na Kaka walitolewa pia uefa hatua ile ile 16 bora wakitolewa na Olmpic Lyon.

2010/2011: Huu msimu wakaamka baada ya kumchukua Mourinho kuwa kocha wao mkuu na alifanikiwa kwa kiasi fulan kuwarejesha katika reli ambapo safari hii walichukua copa de la rey wakimfunga Barcelona na pia walitolewa nusu fainali na Barcelona.

Baada ya hapo Madrid ikarud kwenye njia naweza kusema hivyo msimu uiofuata wakachukua La Liga baada ya kuukosa kwa muda mrefu na pia wakatolewa na Bayern kwenye nusu fainali, Madrid ikaendelea kufanya vizuri na kuingia hatua ya nusu fainali misimu 8 mfululizo.

Madrid sasa imechukua ubingwa wa Ulaya mara 12 jambo ambalo si kawaida ila kwa Madrid wenyewe wameshazoea hali hiyo ya makombe kwana 1956-1960 waliingia fainali 5 za Ulaya na kuchukua makombe yote matano ikiwa ushindi wa 7-3 dhidi ya Frankfurt ambapo Di Stefano aling'ara sana.

Madrid anawinda taji lake la 13 ambapo atacheza na Liverpool huko Ukraine usiku wa May 26, ni mechi ya kukata na shoka ambayo itaamua nani mbabe wa michuano hii kwa msimi huu, Liverpool sio timu ya kubeza katika michuano hii kwan imechukua ubingwa mara 5 na mara ya mwsho walichukua kule Antartuk kule Uturuki baada ya kuwashangaza Wataliano wabishi AC Milan baada ya kuwa nyuma kwa 3-0 na kurudisha zote na kushinda kwa mikwaju ya penati.

Hii Madrid sasa hivi inapofikia michuano ya Ulaya ni nyumbani kwao hivyo wameweza kujiimalisha na kutafuta taji lao la 13. Mwalimu Zidane anafahamu michuano hii ameshachukua kama mchezaji na pia amechukua mara mbili kama kocha hivyo sio mgeni kwenye michuno hii, Real Madrid kutoka kuhangaika miaka 8 hadi kutawala kwa miaka 8 sio kitu rahisi... Heshima kwenu Madrid kila la heri katika taji lenu la 13..
[HASHTAG]#Martinez[/HASHTAG]
 
Mkuu, mimi heshima ya pekee niipeleke kwa Jose Mourinho, huyu bwana alifanikiwa saaana miaka ya nyuma kuipunguza makali Barca.
 
Mkuu, mimi heshima ya pekee niipeleke kwa Jose Mourinho, huyu bwana alifanikiwa saaana miaka ya nyuma kuipunguza makali Barca.
Kweli alipokuja yeye basi utawala wa Barca ukapungua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…