Heshima yako Mkuu

Heshima yako Mkuu

BRN

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2013
Posts
5,188
Reaction score
6,633
Wadau habari.

Kuna hizo salamu kutoka kwa vijana wa siku hizi ambao kwao kusalimia kwa kusema Shikamoo ni shida. Utawasikia wanakuambia Heshima yako Mkuu, kwa kweli mimi nashindwa niwajibu nini.

Je, wewe imeshawahi kukutokea? Je, unajibu vipi?
 
Vyovyote vile utakavyoitikia halafu me nashangaa sana watu wanavyoweka kipaumbele kwenye salaam

Kuna wengine wanataka uwasalimie asalaam aleykum ili kuonyesha upo upande wao yaani salam imekua kama ndiyo kipimo cha utu
Kazi kwelikweli
 
Unapenda kuamkiwa "Shikamoo"?
Naichukia salam ya shikamoo kama ukoma. Kuamkia na kuamkiwa.

Nataman duniani kote salam ingelikua moja tu: Assalam Aleykum.
 
Mkuu salamu ni kitu cha muhimu sana kwa kuanzisha mazungumzo..uzuri wa salamu ukisalimiwa uitikie na ndio maana nimeuliza naitikiaje?
 
Unapenda kuamkiwa "Shikamoo"?
Naichukia salam ya shikamoo kama ukoma. Kuamkia na kuamkiwa.

Nataman duniani kote salam ingelikua moja tu: Assalam Aleykum.
Kwahiyo ukiambiwa Heshima yako huwa unajibuje?
 
Kama na hili nalo limeanzishiwa uzi jukwaani, basi JPM atakumbukwa sana, kama tu alivyosema: ^Ndugu zangu, najua mtanikumbuka kwa mazuri, siyo kwa mabaya!^ Nilimsikia last year akiikata ileeeeeeee ^Shikamoo^ ya Zenj 🙂
 
Back
Top Bottom