Richard mtao
JF-Expert Member
- May 13, 2018
- 262
- 361
Kwa sehemu kubwa hisia tunaweza kuzielezea kama kiashiria kinachokutahadharisha au kutupa msukumo juu ya jambo fulani.
Hisia zinaweza kukuepusha na majanga lakini pia zinaweza kukupeleka katika majanga makubwa yatayopelekea majuto katika maisha yako yote.
Fikiria ni jambo gani baya limewahi kukutokea katika maisha yako na kumbuka vizuri, je kabla ya kulitenda jambo hilo hukupata hofu au wasiwasi?
Kama ulipata hofu au wasiwasi au uzito wowote, ni kwamba hisia zako zilikuwa zimeshatambua kwamba unachofanya sio chema kwako na ndio maana ulikuwa unapata uzito fulani ivi kabla hujafanya.
Nnachojaribu kukieleza ni hapa kwamba, Kabla hujafanya jambo lolote sikiliza hisia zako juu ya jambo hilo, watu wengi tunapuuzia hisia zetu tukidhani tunaweza kufanya kila kitu kwa uelewa wetu huu wa kawaida hali ambayo wengi wetu tunaingia katika matatizo ambayo yanatupelekea kusema "ningejua".
Mwenyezi Mungu alipomuumba binadamu alimpa uwezo mkubwa sana kiasi kwamba hakuna kati yetu anaeweza kudhani ni uwezo kiasi gani lakini baadhi ya mambo yaliyo katika maisha yetu ya kila siku yanaonesha viashiria ambavyo vinaonesha uwezekano wa mwanadamu kuwa na uwezo mkubwa sana, miongoni mwao ni hisia zetu juu ya mambo fulani.
Hivyo unapopanga kufanya jambo lolote mshirikishe Mungu alafu sikiliza hisia zako pale unapoanza utekelezaji, Wakati mwingine Mungu anajibu maombi yetu moja kwa moja kupitia hisia zetu lakini kwakua wengi tunazipuuza na kudhani ni wakamilifu tunazipuuzia hali ambayo inatupelekea kupotea kabisa kwenye game.
Ukitaka kuelewa nguvu ya hisia chukulia mfano wa hisia za mapenzi, watu wanapopata hizi hisia miili yao husisimka na hatimae kutamani kufanya ngono kwa namna yoyote ile. Sasa kinachomfanya mtu atamani kufanya ivo ni nini?
Jibu ni msukumo unaotokana na msisimko wa mwili na homoni zake. Vivyo hivyo kabla hujatenda jambo hisia zinasisimua fikra zako kurejea uamzi wako ili usipatwe na matatizo hapo baadae, sasa hali hii ikikutokea usiipuuzie kabisa tumia akili yako kufikiri mara mbili faida na hasara za jambo hilo maana hiyo itakupa uhakika juu ya unachotaka kukifanya.
Uzuri ni kwamba hisia hazijawahi kumdanganya mtu ni vile wengi wetu hatuziskilizi na sio wavumilivu.
Mfano; "Mtu anaaamini akikamilisha leo jambo fulani litampa faida kubwa na kumsaidia leo" Huu si ukweli hata kidogo unaweza kudhani dili ulilopewa leo ndio litakutoa kimaisha ivyo ikakufanya ufanye kila lililo ndani ya nguvu yako ilimradi tu utekeleze dili hilo lakini kumbe ungejipa muda wa kutafakari vizuri bila papara wala haraka ungeweza kufanya maamuzi mazuri zaidi yatakayo kunufaisha leo na hata kesho na kukuweka salama.
Somo kuu: Sikiliza hisia zako Muda wote ndio kinga yako ya awali.