HESLB: Baada ya Rais kafuta retention fee-6%-heslb tunaomba statements mpya

HESLB: Baada ya Rais kafuta retention fee-6%-heslb tunaomba statements mpya

WAZO2010

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2021
Posts
1,615
Reaction score
3,784
Leo May, 1, 2021. Rais Samia S. Hassan ametangaza kufuta riba ya retention fee ya 6% (Riba ya wizi). Awali tulilipa 10% kama riba ya thamani yote; japo wao waliita penati. Ukweli una bakia kuwa ni riba tu. Na 6% kama retention fee (riba ya kutunza thamani ya fedha). Na makato kwa ujumla yalikuwa 15% ya Gross Salary.

Riba ya 10% ina jumuisha faida hasa kwa mabenki, kutunza thamani ya fedha na athari yoyote ya hasara kibiashara, mfano mnufaika kufariki bila kulipa. Hivyo 6% ilikuwa covered ktk riba ya 10%. Hii 6% ulikuwa ni wizi tu kuziba Mapengo ya wizi wao. Hata ukienda CRDB, NBC, nk uta kopa 8M wata piga na riba mfano 15%, jumla itakuwa mil 12 mfano. Hili deni litapungua kadiri ulipavyo.

Tofauti na huu wizi kwa maskini. Tena wizi wa Serikali kwa watu maskini walioshindwa kulipiwa na Wazazi/walezi wao. Una lipa Million 1.4 kwa Mwaka. Then, mwaka huohuo, retention fee ina ongeza deni lako kwa laki 3. Binafsi sijawahi shuhudia duniani Mkopo wa Kijinga kama huu!!

Hivyo basi baada ya msamaha wa Rais. Kwa ambao tuna lipa bado na ambao hawaja anza kulipa au wanufaika wajao tuna omba INVOICE mpya za Penalt 10% pekee. Nyie kutoka 8% kwenda 15% mlifurahi na kuanza kukata immediately. Pia mikopo ya 2005 hadi 2011 hawa kupaswa kuwa kusthiriwa na sheria hii mpya ila mlikiuka sheria , kanuni na mikataba yao na kuwajumuisha pia. Hivyo hivyo tunaomba Invoice mpya za madeni mapya.

Muosha nae huoshwa! HESLB hawakawii kuleta siasa na janja janja nyingii. Angalizo: hii mikopo ni pesa za kodi zetu, ndg zetu, kaka, baba, mama na wajomba na Shangizi zetu siyo mali yenu. Msijifanye eti mna uchungu sana na faida kwa Loan Board kisa nyie mna mishahara na maposho makubwa. Na mna wasomesha watoto wenu bila Mikopo.

Tunaomba Invoices Mpya.
 
Vipi kwa wale ambao wameshalipa, maamuzi mengine yanatakiwa yaangalie hilo pia.
 
Yangewezekana haya na Jiwe alias mheshimiwa Mungu?

Hiiiiii bagosha!
 
Inabidi watoe invoice mpya ambayo ina deni halisi la mwanzo na penalty yake ya 10%, hizi pesa walizoongeza kwa 6% kila mwaka wazitoe. Ila nna mashaka kama watafanya hivo, sasa hivi watakuja na maufafanuzi yao.
 
Mimi nauliza kuna mtu anadaiwa 5430000, kisha akaekewa 10% ya deni hilo, kisha akawekewa na pesa za field kama 150000, kisha akawekewa kabisa retation fee kama 4070000. Na ameshalipa kama milioni sit. Sasa hiyo milioni 4 za RF zilipatikanaje, kisha je kwa kuondoshwa na rais ndo inatoka yote au vipi
 
Naamini washarekebisha. Aisee sasa ni mserereko tu ni mwendo wa kulipa 30,000 nitamaliza deni nimezeeka. Lazima serikali ifidie elimu yangu kwa huu utaratibu.
 
Back
Top Bottom