HESLB, Chuo Kikuu Tumaini (Iringa) wafanya ufisadi wa kutisha

HESLB, Chuo Kikuu Tumaini (Iringa) wafanya ufisadi wa kutisha

Didia

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2010
Posts
719
Reaction score
260
Ndugu wana jukwaa katika hali ya kushangaza maafisa wa bodi ya mikopo kwa kushirikiana na uongozi wa chuo kikuu cha Iringa zamani kikijulikana kama Tumaini wameamua kukata hela za wanafunzi wanao fadhiliwa na bodi chuoni hapo kinyume na mikataba kati ya wanafunzi na Bodi.

Katika sakata hilo wanafunzi wa mwaka wa pili na watatu wamejikuta katika hatari ya kupoteza kati ya shilingi 150,000 hadi 300,000 kufidia wizi huo. Baada ya kutafuta taarifa bila mafanikio kutoka katika uongozi wa chuo na kujaribu kuhoji uhalali wa swala hilo leo tarehe 5/11/2014 wanafunzi hao wamekumbana na vitisho vikali kutoka kwa Naibu makamu mkuu wa chuo akiwataka kuufyata au vinginevyo watakumbana la rungu la utawala.

Aidha tofauti na ilivyo zoeleka mpaka sasa uongozi wa chuo umekataa kata kata kutoa orodha inayo onyesha kiwango halisi cha ada inayo tegemewa kulipwa na bodi mwaka 2014/2015 ili wanafunzi wasaini ada hizo kwa madai kwamba chuo kina mamlaka ya namna gani kiendeshe mambo yake!

Swala lenyewe liko hivi:

1. Wanfunzi walipata ufadhali wa bodi ya mikopo (kwa mwaka 2012/2013 na 2013/2014) kwa mkataba wa kulipiwa ada 750,000/- ; 1000,000 au zaidi kutegemeana na matokeo ya kipima uwezo ( Means Testing)

2. Katika miaka iliyo tangulia Wanafunzi wameendela kulipiwa viwango hivyo na Bodi na wao kutakiwa kujazia tofauti

3. Katika hali ya kushanganza kwa mwaka huu wa masomo 2014/2015 wanafunzi wamekuta viwango vya ada inayo lipwa na bodi vimepunguzwa kwa kati ya sh. 150,000 na 300,000 na hivyo kutakiwa kulipa tofauti hiyo. Wamefanya kila linalowezeka kutafuta maelezo bila mafanikio


Kwa kutumia jukwaa na mimi kama mdau wa kupinga dhuruma na ufisadi nawasilisha taarifa hii ili tuwasaidie kupaza sauti na kukemea huu wizi


Didia

Nawasilisha

 
Chuo kikuu cha Iringa mambo yao yako ovyoovyo sana, wamejazana wahehe na wengi viwango vyao vya elimu ni magumashi na wananyodo sijapata kuona, tunaomba mbadilike jamani icho ni chuo kikuu.
 
Chuo kikuu cha Iringa mambo yao yako ovyoovyo sana, wamejazana wahehe na wengi viwango vyao vya elimu ni magumashi na wananyodo sijapata kuona, tunaomba mbadilike jamani icho ni chuo kikuu.

Wamefulia balaa. Usitegemee mabadiliko yoyote maana masekretari wengi kuliko walimu so wanatafuta mishahara ya kuwalipa. Poleni ila komaeni mpaka kieleweke wasikifanye chuo kuwa cha kata wahuni hao
 
Kile chuo kina tatizo kubwa la uongozi....kimejaa ukabila na mambo mengi ya kienyeji
 
Mambo yanapelekwa kienyeji sana pale, kila mtu anajifanyia lake, wabadilke kwa kweki
 
Hiyo ni kawaida kutokea Sekomu pia Mambo km hayo huonekana maranyingi hili suala c uongozi Bali ni bodi yenyewe
 
Kheeee wakat wengne wanaongezewa ada wengine wanapunguziwa??? Hii ni ligi
 
Kweli kabisa Sisera,Masekretari kwenye kile chuo ni wengi sana na wana nyodo kama ndo wenye chuo, ukiingia kwenye ofisi za utawala wengine kutwa nzima nikubigastori tu, chuo kimeanza kupoteza ule ubora wake wa zamani
 
wakuonyeshe bodi imelipa ngapi ndipo ulipe. lipa kienyeji bodi wakianza kukata hela yao ndo ntajua
 
mi binafsi cjakupata mkuu, hujaeleza ni kiac gan cha pesa kilicho ibwa, lini, wapi, na ktk mazngra gan
 
Hasara ya mechi za ugenin hizo!!! Bora waliamshe kabisa mpaka kieleweke!!
 
Kwa ninavyowafahamu wale jamaa ni wahuni waliopitiliza, wengine wamejificha kwenye kichaka cha dini kufanya uhuni na wizi ulipitiliza, ukabila, undugunisation na mengineyo.

Walimu nao wanateseka na kulalamika lakini wafanyeje, kila mtu amejichokea zake.
 
Kweli kabisa Sisera,Masekretari kwenye kile chuo ni wengi sana na wana nyodo kama ndo wenye chuo, ukiingia kwenye ofisi za utawala wengine kutwa nzima nikubigastori tu, chuo kimeanza kupoteza ule ubora wake wa zamani

Kila bosi ana ndugu zake pale, mara mtoto wa mchungaji, mke wa mchungaji, mtoto wa mwinjilisti, mara wa Image mara wa Dabaga, mdogo wake fulani, dada yake fulani, uhehe uhehe tu uwajibikaji hauwezi kuwepo kwa namna hiyo. Administrative staff wako wengi na wana mishahara mikubwa kuliko Academic ndio maana wana nyodo. Chuo kinaendeshwa kwa mtindo wa "BORA LIENDE"
 
mnisamehe wa tumaini ila hcho chuo ni kibovuuuuuuu
bora ht form six leaver
 
Kufanya mgomo pale ni vigumu, serikali ya wanafunzi yenyewe haina sauti ni kama inapokea maagizo ya ifanye nini kutoka utawala, ada ya umoja wa wanafunzi ni tsh elfu 18 kwa chuo kile tofaut na vyuo vingine, na haieleweki zile fedha zinatumika vipi
 
Back
Top Bottom