Great thinkers, let us think as great thinkers.
Miaka kadhaa iliyopita sera ya mikopo ilikuwa kwamba mwanafunzi atakayefaulu vizuri masomo ya sayansi atapewa mkopo 100% Hii ilitokana na ukweli kuwa taifa lilianza kukosa wataalamu wa sayansi na watoto walipoteza moyo wa kusoma masomo hayo.
Ni ukweli usiopingika kuwa shule nyingi za kata hazina walimu wa kutosha na hasa wa masomo ya hisabati na sayansi. Mbali ya kukosa walimu pia vifaa na vitabu vya sayansi hawana.
Kutokana na hayo basi, wanafunzi wengi waliofaulu sayansi na hisabati watakuwa wanatokea katika shule za binafsi.
Wazazi wengi walijinyima kuwasomesha shule za binafsi. Nawafahamu waliouza nyumba na mashamba; wakabakiza kidogo tu kwa ajili ya kujikimu wakijua kuwa mtoto akimaliza kidato cha sita tu na kufaulu, then anapata mkopo na kuendelea.
Leo hii ghafla sera imebadilika na kuwanyima mikopo waliofaulu sayansi. Je ule upungufu wa wataalamu umekwisha?
Ikumbukwe pia kuwa vyuo vinavyosomesha wataalamu wa kisayansi vina ghrama kubwa. Ebu fikiria wanaosomea udaktari au masomo yanayohusiana na hayo, gharama zikoje ukilinganisha na wanaosomea arts. Halafu fani kama hizi ndizo hazipewi mishahara mizuri.
Wakati fulani niliwaambia wanafunzi wasomee uhasibu kijana mmoja akauliza, hivi mhasibu na mkurugenzi nani ana mshahara na marupurupu zaidi ya mwenzake? Nikamjibu kuwa ni mkurugenzi. Akaniuliza tena, sasa kuna sababu gani kujiumiza kwenye mahesabu halafu nije kupata maslahi duni?
Alizidi kunitolea mifano ya madkatari wanaokimbilia kwenye ubunge.
Leo hii hata mikopo ambayo ilikuwa ni kivutio kilichobaki, mnaiondoa?
Back-crash ya suala hili inaweza kuanza kuonekana as early as next year.
Kumbe ni afadhali mwanafunzi akasoma arts ambayo inapatikana kwa gharama nafuu katika shule za kata, na akapata mkopo (hata kama hatapata mkopo, bado gharama ni nafuu kuliko wa sayansi)
Mbali na hilo, wako wanafunzi waliosoma shule za serikali tangu primary, wamechaguliwa kusomea mambo ya uganga na hakupata mikopo!
Hakika kuna matatizo katika mfumo mzima wa elimu - hakuna consistency, Hali hi inaonekana hata kwenye mitaala. Utaona mitaala inabadilishwa mara kwa mara na kutungiwa mitihani immediately!