Muntu Ya Pori
JF-Expert Member
- Jun 25, 2013
- 222
- 64
Wadau wa jf nimetoka heslb katika kufuatilia mkopo,walichokisema ni kwamba wale waliokosea kujaza form zao na ni priority kozi ndio watakao angaliwa. Tukamuuliza walioandikiwa eligible but budget exhausted na wale not eligible completed three or more yeas back japo wangine sio kweli, wamesema hao hawatafanyiwa kazl(no loan). Ninawasiwasi kwamba loan bodi wameidanganya serikali kwa kuwaambia waliokosa mkopo form zao zilikuwa na matatizo wakaacha sababu nyingine nyingi. Wanadai kwamba hao waliokwenye list(waliokosea) ndio serikali imewambia wawashughulikie wengine no loan at all, hata kama uliambiwa budget imeisha. Kama serikali ndio imeamua hivyo kuna kila sababu ya waziri mwenye dhamana kuwajibishwa, kwa sababu kawaacha watu ambao wana haki na form hazikukosewa kawachukua watu ambao huenda hata vigezo vingine vya kupokea mkopo hawana( watu wao na labda wenye bahati zao). Mfano kuna watu wamechaguliwa Priority kozi lakini majina hayapo kwa ile orodha na wameambiwa hawatapata mkopo,wafanye nini jamani?. Harakati zimeanza tena upya,tunaelekea tena wizarani kuuliza kwa nini wamewaagiza bodi kuwashughulikia waliokosea form na si wale wenye vigezo vya kupata mkopo bila kuangalia alikosea au hajakosea, ni priority au ni non. Wahanga wengine mtuunge mkono,serikali uwezo inao wa kutupatia mkopo wanafunzi wote vyuo vikuu ila wanaendekeza sana umimi( Wachache wanakula na kufaidi nchi) masikini tunasubiri kipindi cha uchaguzi tuwachague tena waendelee kutunyanyasa. Niulize, hivi haiwezekani kuwatoa hawa jamaa madarakani au wananchi wote tunafurahishwa na wanachokifanya?