Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Fred Ngajiro maarufu kama Vunjabei ameonyesha mtandaoni barua ya kumaliza kulipa deni la ufadhili wa masomo ya digrii ya kwanza aliyopewa na bodi ya mikopo ya wanafunzi wa vyuo vikuu(HESLB) huku akiwahamiza wengine kufanya hivyo pia.
Kama barua hiyo inayosambaa mtandaoni ni ya kweli basi inadhihirisha udhaifu mkubwa wa mfumo wa HESLB katika kukusanya madeni yake. Kuna vijana wengi waajiriwa ninaowafahamu wenye kipato kidogo sana kuliko Fred waliomaliza miaka 10 iliyopita na waliopata mkopo mkubwa kuliko Fred ambao wamemaliza kulipa mikopo yao muda mrefu kuliko yeye.
HESLB inahitaji kufikiria namna mpya ya kuhakikisha sio waajiriwa tu ndio wanaopewa mzigo wa kulipishwa kwa haraka deni la HESLB bali hata wafanyabiashara binafsi. Pia hili linaleta maswali kama Vunjabei amekuwa akiripoti mapato yake kwa usahihi TRA miaka yote hiyo na hiyo milioni 7 ndio iliyopatikana kwa yeye kuwa anakatwa 15% kwa muda wote huo katika mapato yake.
Pia soma Fred Vunjabei amaliza deni la mkopo chuo (HESLB)