HESLB na watu wa DIPLOMA.

Fulugobe

Member
Joined
Sep 30, 2013
Posts
21
Reaction score
4
Nikiangalia kwa uzoefu wangu ktk suala hili la mikopo, naona wazi kuwa HESLB huwa haitupi kipaumbele sana watu wa diploma japokukuwa idadi yetu huwa ni ndogo ukilinganisha na wale wa kidato cha sita. Nakumbuka mwaka 2011 nilichaguliwa UDOM-BSc. Applied Geology wakaninyima mkopo nikaahirisha kusoma. Mwaka huu tena nimechaguliwa UDSM-BSc. in Geology na mkopo nimekosa kabisa. Na ni wengi wa diploma tumetengwa tena mwaka huu na HESLB kana kwamba sisi tuna uwezo wa kujisomesha. Ipo haja ya kufanya kitu hapa, NACTE nao wanapaswa kutuunga mkono hapa.
 
Ni kweli mkuu, mdogo wangu kakosa, amepata Mzumbe HR. Watu wa diploma wanadhani labda ni wafanya kazi which is a wrong perception.
 
mimi mwenyewe nimeandikiwa did not secure hv hii luga inamaanisha nini? maana nimechaguliwa chuo cha tia dsm bachelor in accountancy. nipo njia panda kulisongesha. hawa nacte ni taasisi telekez sana kwan kn koz za non prioty jamaa yangu amepata mkopo, yy amemalza 4m6.
 
Ni kweli mkuu, mdogo wangu kakosa, amepata Mzumbe HR. Watu wa diploma wanadhani labda ni wafanya kazi which is a wrong perception.

Haiko sahihi hata kidogo kwa wanachokifanya. Mtu anachaguliwa course prority, na vigezo vyote vya kupata mkopo anavyo kisa kasoma miaka ya 2002, 2004 au 2006. Mimi nina historia ya kukosa mkopo tangu 2005 nilipomaliza A' level. Nikona nisipoteze wakt nikajiunga na diploma kwa ada za bei ndogo tu. Ila naona upepo unazidi kuwa mbaya upande wangu.
Jamani wahanga wenzangu wa hili mnalichukuliaje, tuendelee kukaa kimya tu?
 
Mi nadhan bodi toka ianzishwe hakujawa ufuatiliaji wa kweli je watu wanaopata na fani zenyewe,wanaandika priority lakn watu wanakosa mikopo mi nadhan wanatakiwa kumulikwa mi nina was2 nao.
 

mi nadhani wanatuhija tupige mzigo na diploma(kada ya kati) zetu ili kama utahitaji degree uipate kwa juhudi zako za kuhifadhi mshahara,sasa shida ni kazi zenyewe hazipatikaniiii na ukipata mshahara njiwaaa na mwisho wa siku unazeeka na diploma yako,
 
mi nadhani wanatuhija tupige mzigo na diploma(kada ya kati) zetu ili kama utahitaji degree uipate kwa juhudi zako za kuhifadhi mshahara,sasa shida ni kazi zenyewe hazipatikaniiii na ukipata mshahara njiwaaa na mwisho wa siku unazeeka na diploma yako,

Wengine wenye diploma wanapata, wengine chali. Angalau basi hata kama wangetunyima tuition fee na hizo nyingine wangetupa tungejua nini cha kufanya mbeleni. Sasa BSc. Geology miaka 4 UDSM almost 16mil bila mkopo?? Ndoto ya elimu ya juu inaanza kunifutika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…