Leembaswagger
Senior Member
- Aug 1, 2012
- 100
- 34
Kwa muda mrefu hapa nchini tumekuwa tukimtafuta mchawi ni nani anayeharibu ustawi wa wanafunzi wa elimu ya juu hapa nchini (hasa wa kike),lakini kwa kipindi hiki kifupi tangu nilipofika hapa chuoni (Mbeya University of Science and Technology,MUST zamani MIST) nimepata jawabu kuwa ingawa wapo baadhi ya wanafunzi wa kike wenye hulka ya umalaya lakini kwa kiasi kikubwa umalaya wao unachangiwa na ukosefu wa pesa,kwa mfano:- chuo kimefunguliwa tarehe 15 Oct mpaka leo hii bado mikopo yetu wanafunzi hatujapatiwa,fikiria kwa mtoto wa kimasikini aliyetokea DAR hana hata ndugu mmoja Mbeya mahitaji yake ya kila siku atayapata wapi?,na hiki ndiyo chanzo kikubwa cha umalaya,izingatiwe kuwa Mbeya ni mkoa wa pili kwa maambukizi ya virusi vya Ukimwi baadhi ya wanafunzi waathirika wanaoletwa vyuoni (a.k.a watoto wa mama Salma) hali inazidi kuwa mbaya,serikali iliangalie hili kwa macho angavu.Naomba kuwasilisha